Mtu mmoja amefariki dunia mara baada ya
kujinyonga na watu wawili wamekamatwa wakiwa na misokoto ya madawa ya kulevya
314.
Akithibitisha kutokea kwa matukio
hayo kamanda wa polisi mkoani hapa
alisema kuwa tukio lakwanza lilitokea maeneo ya Engoserngiu katika halmashauri
ya jiji la Arusha ambapo mtu aliyejulikana kwa jina la Bw. Tisiano Likiwilike(30)
makazi wa Engosengui alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ambapo
8ilifungwa kwenye mti uliopo pembeni mwa nyumba aliyokuwa anaishi.
Alisema kuwa uchunguzi wa awli wa polisi
umebainishwa kwamba siku ya tarehe 20 muda wa saa 11:jioni marehemu aliondoka
nyumbani kwake bila kuaga na kuelekea kusiko julikana na tarehe 21 muda huo wa
saa 2:30 asubui baadhi ya mashuhuda
waliukuta mwili huo umeninginia juu ya mti.
Alibainisha kuwa mashuhuda waliamua
kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi ambapo askari waliokuwa doria
maendeo ya karibu na tukio hilo na
walipofika eneo la tukio waliukuta mwili huo na walipofanya uchunguzi katika
chumba cha marehemu walikuta karatasi juu ya kitanda chake iliyoandikwa ujumbe
usemao asilaumiwe mtu yeyote juu ya kifo changu kwani maisha n ya duniani
yamenishinda sina thamani tena.
Kamanda amesema umeifadhiwa katika
chumba cha kuifadhia maiti cha Mounti
meru kwa ajili ya uchunguzi zawa
daktari na jshi la polisi mkoani hapa linaendelea na upelelezi wa tuki hilo.
Wakati huo huo watu wawili wamekamatwa
na madawa ya kulevya aina ya baingi 314
latola eneo la unga Limited lililopo katika halmashauri ya jiji la Arusha .
Aliwataja watu hao waliokamatwa kuwa ni Bi.
Linah Christop pamoja na Elizabety Chirstoph ambao walikutwa na misokoto hiyo katika eneo la soko mjinga Ungalimeted
Alibainisha kuwa mafanikio hayo
yalitokana na taarfa zilizotolewa na raia mwema kwa jeshi la ambapo mara baada
ya taarifa hiyo askari hao walikenda moja kwa moja katika nyumba ya watuhumiwa
na kupekuwa ndipo walifanikiwa kupata bangi hiyo iliyokuwa imehifadhiwa kwenye
mfuko wa Plasitikc maarufu kama Malboro
Alibainisha kuwa mara baada ya mahojiano
watuhumiwa ho walikiri kwamba walikuwa wamehifadhi bangi hiyo kwa ajili ya
kuuza na mpaka hivi sasa jeshi la polisi limeshawafikisha watuhumiwa hao
mahakamani