wananchi wakikwa wanamsikiliza Mlezi wao wa polisi jamii kwa makini
ofisa wa polisi jamii mkoa wa Arusha Mary Lugola akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Elerai
POLISI Mkoa wa Arusha, umewataka wananchi kuwafichua wahalifu
mapema kabla ya kufanya uhalifu.
Ofisa Mkuu wa Polisi Jamii wa mkoa, Mary Lugola, ambaye pia
ni mleziwa polisi jamii Kata ya Elerai, alisema hayo wakati akitoa mafunzo
kuhusu polisi jamii kwa wananchi wa kata hiyo.
Alisema kila mwananchi anatakiwa kuwafichua wahalifu ambao
wanaishi karibu nao au mtu ye yote ambaye anamuonea wasiwasi kuwa ni muhalifu
au anatarajia kufanya uhalifu kabla ya madhara hayajatokea.
Alisema polisi watatoa ushirikiano wa hali na mali iwapo mwananchi atatoa taarifa kuhusiana na uhalifu wa aina yoyote.
“Ukiwa una taarifa yo yote ya uhalifu iwe ni mtu anauza
bangi au anauza gongo au anataka kwenda kuiba sehemu, toa taarifa kwa polisi na
sisi tutamfichua mapema na kumchukulia hatua kabla ya mtu huyo hajafanya tukio
lolote la uhalifu,” alisema.
Kuhusu malalamiko ya unyanyasaji yanayofanywa na Wamasai kwa
maelezo ya kutekeleza mila zao, Mary alisema polisi kawa kushirikiana na polisi
jamii watahakikisha kwamba unyanyasaji huo hauendelei kufanywa kwa kigezo cha kudumisha
mila.
Katika kutekelea mila za Kimasai, hususan, jando, inadaiwa
kuwa baadhi yao wananyanyaswa kwa kuvalishwa mabati, magunia, kuzomewa na mambo
mengine kadhaa.
“Napenda kuwaambiwa wananchi hawa ambao wamekuwa wakifanyiwa
vitendo hivi kuwa ili kumrahisishia polisi
kazi yake na ishughulikiwe mapema ni lazima mtu yule amfahamu mtu aliye
mfanyika kitendo hicho japo kwa sura ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema.