WATOTO NANE WAFA MAJI HUKU WAWILI WAMENUSURIKA



Watoto kumi(8) wa shule ya shule ya msingi Piyaya iliyopo katika tarafa ya Sale  kata ya Malambo katika kijiji cha Piyaya kitongoji cha Madukani wanaofiwa kufa maji na wengine wawili kunusurika kufa .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa tukio hilo lilitokea febuary 27 mwaka huu majira ya saa 11:20 jioni ambapo  mvua kubwa  ilionyesha ilisababisha watoto kumi wa shule hiyo kuofiwa kufa maji. 
 
Alisema kuwa watoto hao ambao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi  Piyaya wanaofiwa kufariki dunia wakati walipo kuwa wakivuka mto Lusokutane uliokuwa umejaa maji .

Magessa alisema uwa kufuatia taarifa hiyo ya watoto hao kuhofiwa kufa maji kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngorongoro ilifika katika eneo la tukio kwa kushirikiana na uongoazi wa kijiji na wananchi ndipo ikagundulika kwa kati ya hao watoto kumi watoto wawili waliokolewa wakiwa hai na watoto nane wamefariki dunia .

Aliwataja watoto ambao miili yao ilipatikana na imeshazikwa  kuwa ni Nemao saragi (11),Rapaine Lekima (12),Kiasiaya Kima (12),Olanana Lekima (13) pamoja na Lekinyori Lemasa(11) wote wakiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Magessa aliwataja watoto ambao bado hawajapatikana na wanaofiwa kufa kuwa ni pamoja Nanyangusi Ndalau msichana ((12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano,Lekinyori Lemasa mvulana (11) na nimwanafunzi wa darasa la tatu na watatu ni Sileti kakea mvulana (9)na nimwanafunzi wa darasa la pili.

Mkuu wa mkoa alisema  walionusurika kufa kuwa ni Njiroine Ning'atu mvualana (13) mwanafunzi wa dara la saba pamoja na Mapehu Lekima mvulana (9) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili.

Alibainisha kuwa mpaka sasa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya Ngorongoro kwa kushirikiana na viongozi wa kujiji na wananchi bado wanaendelea na jitihada za kutafuta miili ya watoto ambao bado hawajapatikana .


kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo linasikitisha mno na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi watashirikiana kwa pamoja kutafuta miili ya watoto waliobakia.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post