SERIKALI YATAKIWA KUHAKIKISHA WALIMU WALIOPO MASHULENI WANAFUNDISHWA MAFUNZO MAALUMU KWA AJILI YA WATOTO WALEMAVU

katibu mkuu wa FPCT Elias Sija akiwa anafafanua jambo katika  uzinduzi wa baraza hilo
mwanasheria wa baraza la watoto wenye ulemavu (FPCT) Gidion  Mandesin aliyevaa miwani akitoa mada katika mkutano wa uzinduzi wa baraza la watoto walemavu





SEREKALI  imetakiwa kuhakikisha walimu wote ambao wapo mashuleni wanapata ufundi na ujuzi was kufundisha watoto wenye maitaji maalumu yakiwemo ulemavu.

Hayo yamebainishwa na mwanasheria wa baraza la watoto wenye ulemavu (FPCT) Gidion  Mandesi wakati alipokuwa  akitoa mada katika semina ya wadau wa masuala ya mtoto na ulemavu mkoa wa Arusha iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini hapa.

Alisema kuwa kutokana na kuwa na watoto ambao ni walemavu ambao wamegundulika kwa wingi hivyo serekali kwa ujumla inatakiwa kuhakikisha  kuwa kila chuo cha uhalimu kinafundisha masomo maalumu kwa ajili ya wanafunzi walemavu.

Alibainisha kuwani wajibu wa serekali kuweka mazingira mazuri watoto ambao ni walemavu ikiwemo  kuwawekea shule ,vifaa mbalimbali ,vitabu,maandishi ya nukta pamoja na maandishi makubwa ambayo kni kwaajili ya walemavu wa ngozi.

“unajua mtoto ambaye ni mlemavu iwapo utampatia elimu kwanza itamsadia yeye mwenyewe kwani itamsadia kupunguza upweke ,itamfanya yeye kama yeye mlemavu kujiamini  na pia inaweza kumuezesha kupata skimu  ,kuweza kujitambua yeye mwenyewe  pamoja na kujua wajibu wake katika jamii;alisema Mandesi

Naye afisa maendeleo ya jamii sekretariti ya mkoa wa Arusha Blandina Nkini ambaye ndie Mgeni rasmi wa uzinduzi huu wa Baraza la watoto wenye ulemavu mkoani hapa aliwapongeza kanisa la Pentecostal  kwa kuamua kutoa huduma kwa jamii haswa walemavu  kwa kuzingatia mkataba wa kimataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu ya mwaka 2006 na hali kadhalika katika sera ya taifa la tanzania kuhusu maendeleo na huduma kwa wenye ulemavu ya mwaka 2004 na pia kupita mkataba huo wakimataifa kuhusu haki za watoto walemavu na wakaamua kuanda sera ya watoto walemavu Tanzania .

Alisema kuwa serekali wanaunga mkoanio kanisa pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha azma ya serikali na kanisa ya kuwekeza kwa watoto kwa mstakabali wa taifa la kesho kwani maendeleo ya watoto yanategemea sana na namna gani wanawekeza katika miili ,mioyo ,roho na hata akili za watoto.

Kwa upande wake katibu mkuu wa FPCT Elias Sija alisema kuwa wameamua kuanzisha baraza hili ili waweze kufikiwa na hata walemavu ambao wapo vijijini ambao bado hawajapata huduma kama ambavyo wenzao wanazipata  na hivyo wao kama kanisa wanampango wa kuwafikia hata watoto ambao ni walemavu ambao hawajapata huduma kama vile elimu ili waweze kuzipata kama watoto wengine.

Alisema kuwa kwa kuwa wameamua kuanzisha baraza hili  la watoto wenye ulemavu mkoani Arusha ili kuweza kuwasaidia na watoto wa mkoani hapa ambao wapo vijijini nil walemavu na hawajapata fursa kama hizi na kubainisha kuwa mpaka sasa wameshaanzisha mabaraza kama haya katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Tanga ,Rukwa ,Mwanza ,Shinyanga pamoja na mara na wanampango wa kuanzisha mabaraza haya katika mikoa yote Tanzania.

Alitoa wito kwa wananchi wadau serekali kutoa ushirikiano  wa hali na mali ili kuweza kufanikisha swala ili pia aliwataka wananchi kuwafichua watoto ambao ni walemavu waliopo katika vijiji vyao na kama wataweza wawasaidie kwani ni binadamu kama wengine.

‘nachopenda kuwasihi wananchi wawatoe watoto ambao ni walemavu na wawa saidie wasiwanyanyapae kwani ni binadamu kama wengine wanaitaji kusaidia na nauhakika wakiwezeshwa wataweza”alisema Shija.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post