WANANCHI wa kjiji cha Olkunjwado kilichopo kata ya
Ngarenanyuki wilayani Arumeru
wamemlalamikia mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Loibai kwa kosa la kuuza ardhi kinyume cha sheria
sambamba na kutowasomea mapato na
matumizi wananchi hao.
Wakiongea na Libeneke la kaskazini baadhi ya wananchi
ambao hawakupenda kutajwa majina yao
walisema kuwa mwenyekiti huyo amakuwa na tabia ya kuuza maeneo ya watu wasiokuwa na uwezo kwa mzungu anaeishi
katika kijiji hicho kwa manufaa yake
binafsi Aidha walisema kuwa sheria ya
ardhi inasema ardhi haiuzwi kiholela na hata
kama basi itauzwa kuna asilimia ambayo itaenda serikalini lakini kwa mwenyekiti huyo ni tofauti na sheria hiyo.
Mbali na hilo waliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka jana walimtaka
mwenyekiti huyo kuwasomea wananchi hao mapato
na matumizi kwa ajili ya michango mbali
mbali wanaochanga kijijini hapo lakini hakufanya kama
walivyokuwa wanataka wao.
Waliongeza
kuwa mapato hayo na matumizi waliyoomba kusomewa yanatokana na michango waliyochanga kwa ajili ya shule ya kutwa
ya sekondari ya Momela na hadi sasa
fedha hizo hazijulikani zilipo hali ambayo inawatia mashakani na mwenyekiti huyo ambapo hadi sasa wamekataa kuchanga michango mingine hadi wasomewe mapato hayo
Hata hivyo walimtaka diwani wa kata hiyo
kuitisha mkutano ili waweze kutoa kero
zao kwa kuwa mwenyekiti huyo amekataa kusikiliza kero zao
Aidha libeneke la kaskazini liliweza kuongea na mwenyekiti huyo kwa njia
ya simu na kueleza kuwa hajauza ardhi
kinyume cha sheria bali ni makubaliano yao wote waliopitisha
kumpatia mzungu huyo eneo.
Kwa upande wa kuwasomea mapato na matumizi alisema
kuwa alishawaomea mapato na matumizi kwa
kipindi cha nyuma ila mara ya mwisho koramu haikutimia hivyo kushindikana kusomewa kwa mapato hayo