KILIMARATHONI WATANZANIA WAZIDI KUACHWA MBALI


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha kuanzia 20,000/= kwa mshindi wa tatu upande wa wanawake Natalia Elisante, wa mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.

 wazungu bwana walikuja na wanyama wao kukimbia uyu alianza na mpwa wake na kumaliza naye na sisi je

mapacha walinogesha mashindano ya kilimarathon walitumbuiza vipaya mno

Serekali imeshauri kuteuwa vipaji vya watoto wadogo ambao ni wanariadha  ambao wataenda  kupatiwa mafunzo nje ya nchi  ili kuweza kunyanyua mchezo huo .

Hayo yamebainishwa na kocha wa timu ya riadha  nchini Kenya ,ambaye pia ni kocha wa klabu ya rafiki internspot ya nchini humo Reuben Oron wakati akiongea na libeneke hili  wakati alipohudhuria katika mashindano ya Kilimarathoni yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro jijini hapa.

Alisema  mchezo wa riadha kwa nchi ya Tanzania unazidi kushuka siku hadi siku hali ambayo inasababishia watu wengi kushangaa nchi hii.

“mnajua nyie zamani mlikuwa unafanya vyema sana katika mchezo huu wa riadha sasa saivi hamfanyi sijui ndo tuseme hamna makocha au ni kwasababu gani mnadidimia na cha aibu zaidi nchi kama Tanzania ambao ndio wahasisi wa Kilimanjaro marathoni mashindano ambayo yanauthuriwa na nchi mbalimbali mnashidwa kuchukuwa ubigwa kweli katika mita zote nyie wenyeji mnaweza kumwaga kwenye kumi bora akawa mmoja jamani kweli ni aibu kubwa na kama tumeanza hivi uko mbele mtafikia ata kwenye ishirini bora hampo”alisema Oron

Alisema kuwa kutokana na hali hii na kuwaona watanzania ndio waandaaji wa mashindano haya basi tunaona nibora tutoe nafasi kwa nchi ya Tanzania kuleta wachezaji wadogo ambao wanavipaji ili tuweze kuwafundisha na wao warudi katika chati katika riadha.

“unajua sisi tuna klabu nyingi pale nchini kwetu ivyo tunatoa nafasi za vijana ambao wanavipaji waletwe katika klabu zetu na sisi tutawafundisha  ili na Tanzania waweze kushika nafasi za juu za riadha kama sisi wakenya tunavyoshika na kama itashindikana basi tutawaruhusu waje wachukuwe kocha ambaye atafundisha watoto hao wenyevipaji’alisema Oron

Pia aliiasa serekali kuanzisha michezo katika shule za msingi kuanzia chekecheka kwani iwapo watafanya ivyo watasaidia kumjenga mtoto tangu akiwa mdogo huku akisisitiza elimu dhidi ya michezo itolewe kwa walimu wa shule zote kuanzia msingi adi sekondari  na walimu hao wakipata elimu  hiyo sio wakalie tu bali waifanyie kazi na wafundishe watoto.

“Unajua sisi tunavyofanya tunamuandaa mtoto kulingana na umri wake na katika mbio tunamkimbiza kulingana na spidi yake na tunawatoto kuanzia ata miaka minne tunawafundisha na kama mtoto anaanzia kama niseme kilometa 20 atakimbia kulingana na mri wake na tutazidi kumuongezea kilometa jinsi anavyozidi kuongeza spidi”alisema Oron



 katika pita pita ya hapa na pale libeneke likawafuma hawa wadada wakiwa wamepanda juu ya viti wanayarudi ngoma za mapacha watatu katika uchunguzi likabaini ni waandishi kutoka Arusha
 
Wakati huo huo mbizo  za kujifurahisha za kilometa 5 za (Vodacom 5KM fun run) ambazo ni sehemu ya mbio za Kilimanjaro Marathoni zimezidi kujizolea umaarufu na watu wengi rika tofauti kujitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo yaliyofanyika juzi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wa mbio hizo, Rukia Mtingwa katika mbio za mwaka huu jumla ya watu 10,000 wamejitokeza kushiriki kwenye mbio hizo tofauti na makadirio ya kawaida ya kupata jumla ya washiriki 5000 ambacho ndicho huwa kiwango cha juu.

Mtingwa alisema wengi wa washiriki katika mbio hizo kwa mwaka huu zimetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na vyombo vya habari na mvuto wa mbio hizo ambazo huambatana na manjonjo mbalimbali Kutoka kwa washiriki wake na zawadi za kuvutia zinatolewa na Vodacom.

Pamoja na mafanikio hayo Mtingwa alisema wao kama wadhamini wamepata changamoto kubwa katika mbio hizo hasa kwa mwaka huu kutokana na wakimbiaji wazoefu kujitosa kushiriki kwenye mbio hizo badala ya kuwaachia watu wengine ambao riadha sio fani yao.

“Kwa kweli mwaka huu tumekumbana na changamoto hiyo ya wakimbiaji profession kushiriki kwenye fun run ambazo sisi tunaona ni maalum kwa watu ambao riadhi si fani yao kwahiyo kipindi kijacho endapo tutaendelea na udhamini wa mbio hizi itabidi tuifanyie kazi changamoto hii,” alisema Mtingwa.

Aidha Mtingwa alisema changamoto ya kujitokeza washiriki wengi kwao ni faraja kubwa na watajipanga kukubaliana na haki hiyo ili kuendana na mazingira ya ukubwa wa mbio hizo kadiri watu watakavyokuwa wakijitokeza.

Washindi wa mbio za juzi kwa upande wa wanaume ni Gailet Ismail ambaye alichukua na nafasi ya kwanza na kujinyakulia simu ya mkononi aina ya ZTE S- 501,muda wa maongezi wa sh 20,000, modem ya intaneti pamoja na M-Pesa ya Sh 100,000.

Brazil Boay alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa simu, muda wa maongezi, modem ya intanert na M-Pesa ya sh 80,000 wakati mshindi wa tatu alikuwa Fabiano Nelson ambaye naye alipata simu, muda wa maongezi, modem na M-Pesa ya Sh 60,000.

Na upande wa wanawake washindi walikuwa ni Jackline Sakilu, Catherine Iranga na Natalia Elisante ambao nao walijishindia zawadi sawa na zile walizopata wanaume, washindi wengi kuanzia nafasi wanne hadi 10 pamoja na wshiriki walioweza kumaliza mbio hizo nao walipata zawadi mbalimbali kutoka Vodacom.

Huo ni mwaka wa tano tokea Vodacom iwe mdhamini wa mbio za kilometa tano za kujifurahisha (Vodacom fun run) ambazo ni sehemu ya mbio maarufu za Kilimanjaro ambazo mwaka huu zimeadhimisha miaka 10 tokea kuanzishwa kwake.



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post