WAANDISHI ARUSHA WAKUTANA NA MKUU WA MKOA

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anaongea na waandishi wa habari katika kikao ambacho waandishi walimualika kama mgeni rasmi  kilichofanyika katika ukumbi wa hotel ya Bristoni mjini Arusha
 waandishi wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa kwa makini
 baada ya hapo waliamua kupiga picha ya pamoja hapo ni baadhi ya waandishi waliouthuria semina hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa APC Gwandu wakiwa katika picha na mkuu wamkoa
hili ni  kundi lingine ambalo lilipiga picha baada ya kukosa nafasi katika hawamu ya kwanza



kama kawaida mkuu wa mkoa wetu ni mtu mpenda watu anaongea na kila mtu apo alikuwa anabadilishana mawazo na wafanya kazi wa Radio 5 akiwemo mtangazaji mashuhuri mkubwa au waweza sema mpiganaji Devid  pamoja na Ashura Mohamed wote wakiwa wanafurahia siku hii


Katika kikao hichi cha waandishi wa habari wa mkuu wa mkoa kuliongelewa  mambo mengi ikiwemo jambo ambalo mkuu wa mkoa alilisema kuwa waandishi wahabari wafanye kazi kwa kufuata sheria na kanuni pia aliwasihi waandishi hawa kujaribu kuandika habari za ukweli ambazo zinaleta faida kwa wananchi katika uwandishi wao wajaribu kuandika habari zinazo elezea pande zote mbili na sio upande mmoja tu ,

Aidha pia aliwataka waandishi wahabari washirikiane na iwapo wanaenda katika kazi wakiwezeshwa basi wafanye kazi kama walivyokubaliana na wadau nasio kwenda kuchukuwa ela alafu kukaa kimnya pasipo kuandika habari ambayo walitakiwa waandike

Mara baada ya kukaa kikao hicho mkuu wa mkoa aliondoka na waandishi ambao ni wanachama hai wa APC walibakia huku baadhi ambao walikuwa hawajalipa ada yauwanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha wakiwa wametolewa nje.

Nawaliobaki ndani walijadili mambo mengi pamoja na kuifanyia marekebisho katiba ya APC na kupitisha katiba hiyo ambayo wameifanyia marekebisho.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post