MWENDESHA pikipiki aina ya Bodaboda
Hosseni Jumanne(28) mkazi wa Nyunguu mjini Babati amekufa baada ya pikipiki
aliyokuwa akiendesha kuigonga pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na koplo Emanuel
wa polisi wilayani Babati.
Awali kabla ya kutokea kwa ajali
hiyo usiku mashughuda wa ajli hiyo walisema ajali hiyo ilisababishwa na askari
huyo kufukuzana na mwendesha pikipiki huyo na baada ya kumpita alimzuia kwa
mbele na kisha kuigonga pikpiki hiyo akiwa katika mwendo wa kasi na kusababisha
kifo cha mwendesha pikipiki huyo huku askari huyo akiendesha askari huyo
akipoteza fahamu.
Hata hivyo kufuatia ajali hiyo
majruhi wote wawili walikimbizwa kupatiwa matibabu wakiwa katika hali mbaya na
kusababisha kifo cha Hosseni huku Koplo huyo akiwa mahututi na kukimbizwa
kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya misheni ya Kanisa la Kiinjli la
kilutheri ya KCMC iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa polisi mkoani hapa
Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo juzi majira ya saa
6:30 usiku iliyotokea katika barabara kuu inayotoka mjini Babati kuelekea
wilayani Kondoa na kuhusisha pikipiki T116 BNQ iliyokuwa ikiendeshwa na
marehemu huyo na SM 9426 iliyokuwa ikiendeshwa na koplo Emanuel.
“chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa
kasi uliochangia kushindwa kudhibiti pikipiki zao na kusababisha kugongana na
hatimaye kusababisha kutokea kwa kifo hicho pamoja na kuumia vibaya kwa askari
huyu ambaye amepelekwa kupatiwa matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC” alisema.
Kwa upande mwingine baadhi ya
wananchi waliokuwa eneo la msibani wamemlalamikia kamanda Sabas kwa askari wake
kutuhumiwa kusababisha ajali za mara kwa mara kutokana na usumbufu wa askari
hao kuwasababisha usumbufu wa leseni na ukaguzi wa mara kwa mara wenye
mazingira ya kuomba na kupokea kitu kidogo.
“sabas arekebishe askari wake
wamekuwa wasumbufu wamekuwa wakiomba leseni ukishamwonyesha leseni anaichukua
na kutishia kukupeleka kituoni ukibabaika tu anakuomba fedha sasa hili ni
usumbufu unaosababisha ajali za mara kwa mara…wengine wanaleta usumbufu wa
kusimaisha pikipiki za wakulima njia za miguu vijijini wakiwemo FFU”
Tukio hilo ni la tatu Januari 17
mwaka huu askari kanzu mmoja(jina tunalo) wa polisi alinusurika kuuwawa na
wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Bonga baada ya kupata kipigo
kikali toka kwa wananchi waliochukizwa na tabia hiyo ya askari hao na baadaye alikimbizwa
kupatiwa matibabu katika halmashauri ya mji wa Babati.
Licha ya tukio hilo pia siku hiyo
hiyo ambayo hufanyika mnada askari mwingine alimsababishia mkulima mmoja mkazi
wa Galapo kulazwa katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali iliyosababishwa
na askari polisi aliyekuwa akimfukuza kwa madai ya kutokuwa na leseni na
alipomkuta wakiwa katika mwendo alimsukuma na kisha pikipiki hiyo ilianguka na
kumsababishia mkulimahuyo kuvunjika mguu.
Bado wananchi mjini babati wamemtaka
kamanda huyo wa polisi kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa askari wake ambao
wameonekana kuwa kero katika utendaji kazi wao wenye mwelekeo wa kudai kipato
binafsi ambacho kinakwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo pamoja na kiapo
wakiwemo askari wa usalama barabarani,upelelezi na wale walioko kauta.
Hivi karibuni kamanda Sabas
alipoulizwa kuwepo kwa malalamiko hayo aliwataka wananchi kuwafichua kwa
kuwataja majina badala ya kuzungumzia mitaani na kusisitiza kuwa atawachukulia
hatua kali askari watakaokuwa wametajwa katika mwenendo huo ulio kinyume na
maadili ya kazi hiyo.