WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI

Watu watatu wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanamke kuwawa na watu wasiojulikana.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akil Mpwapwa alisema kuwa tukio la kwanza ni la ajali ambapo watu wawili walifariki dunia mara baada yakupata ajali wilayani karatu.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea january 30 majira ya saa 11:30 jioni katika eneo la bashai lililipo katika barabara iendayo Ngorongoro wilayani Karatu.

Alibinisha gari lenye namba za usajili KAW 314 B ambazo ni namba za nchi jirani ya kenya na ni mali ya kampuni ya utalii ya Tome safari LTD lililokuwa likiendeshwa Karen Lovis (24) mzungu  na mkazi wa nchini kenya ambalo lilianguka na kusababisha majeraha.

Alisema kuwa gari hilo ambalo lilikuwa linawatu wawili ambaye aliwataja kuwa ni dereva na mwenzake mmoja aliyejulikana kwa jina la Sebastani Horiama(27) liliacha njia na kuanguka  hali iliyomsababishia dereva huyo na mwenzake kupatwa na majeraha makali yaliyowafanya wakimbizwe katika hospitali ya kanisa la lutherani kwa ajili ya matibabu.

"kwakweli watu hawa walikimbizwa katika hospitali hiyo ya kanisa ya mjini karatu lakini kwa bahati mbaya majeruhi hao walifariki dunia wakati walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo"alisema mpwapwa.

Alisema kuwa miili ya marehemu hawa imeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru.

Mpwapwa alibainisha kuwa katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa ajali hii ilisababishwa na mwendo kasi ambao dereva alikuwa anauendesha gari.

wakati huo huo katika tukio lingine mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Paulina Solomoni anaekadiriwa kuwa na mikaka 35-40 amefariki dunia mara baada ya kukatwa mashavu yote mawili pamoja na kidevu na watu wasio julikana.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea january 30 majira ya saa tano asumbu katika eneo la buruka olasiti katika halmashauri ya jiji .

Alisema kuwa mtu huyo ambaye alikuwa anauza matofali kwa Jackisoni siningo aliuwawa kwa kukatwa mashavu yote na kidevu na watu wasiojulikana na kumfungia ndani kweke kisha wakaondoka

Alisema kuwa mwili huo w amarehemu uligunduliwa na Jackison Saningo akiwa pamoja na fundi ujenzi ambapo walifika katika nyumbani kwa mama huyo kupata cementi ya mafundi lakini walivyofika walikuta mlango umefungwa.

"walifika wakakuta mlango umefungwa wakaita mda mrefu hawakuitikiwa wakashangaa na ndipo waliamua kuvunja mlango na ndipo walimkuta marehemu amejifunika gubi gubi na shuka na walipomuita bado hakuitika ndipo walipoamua kumfunua na kumkuta akiwa anatokwa na damu nyingi huku akiwa amefariki dunia"alisema Mpwapwa.

Aidha alibainisha kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na ndipo polisi waliokuwa doria katika eneo hilo walienda kuuchuku mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya maunti meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi .

'tunaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hili pamoja na watu ambao wamehusika na tukio hilo"alisema Mpwapwa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post