Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ameuwawa na wananchi
wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuvunja grocery na kuiba.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi
mkoani hapa Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea January 25
mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku katika kijiji cha Kiranyi kilichopo katika
halimashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.
Alisema kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la John Raphael
Mrema anaekadiriwa kuwa na miaka 25-30 aliuwawa na wanchi wenye hasira
kali baada ya kutuhumiwa kukvamia grocery
na kuiba.
Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa ambazo jeshi la polisi
zimezipata zinasema kuwa siku ya tukio marehmeu akiwa na wenzake ambao hidadi
yao haijajulikana ambao walishirikiana kuvunja grocery ya mtu aliejulikana kwa
jina la Eva Katapa (26) mfanyabiashara na kuiba vivyaji mbalimbali pamoja na
fedha taslimu kiasi cha shilingi laki 600,000.
“sasa baada ya majambazi hawa kuiba katika grocery hiyo ya
kwanza waliamia katika grocery ingine ambayo ipo jirani ambapo hapo pia
walivunja grill lakini kwa bahati nzuri pale hawakuweza kuchukuwa kitu chochote
baada ya majirani kuamka na kufanikiwa
kumkamata ndugu John Raphael ambapo walianza kumshambulia kwa kupiga
hadi kuuua huku wenzake wakiwa wamekimbia”alsiema Andengenye.
Kamanda wa polisi alibainisha kuwa mpaka sasa hakuna mtu
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la polsisi mkoani Arusha
linaendlea na upelelezi kuwasaka
waliokimbia .
“mwili wa marehemu umehifathiwa katika hospitali ya mkoa ya
maunti meru hadi hapo ndugu wa marehemu watakapo kuja kuuchukuwa na pia
upelelezi unaendelea “alisema Andengenye.