JAMBAZI AUA POLISI ARUSHA, PIA AMJERUI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI

kamanda wa polisi mkoani Arusha Thobias Andengenye Akiwa anaonyesha silaha aina ya SMG ambayo mmoja wa majambazi alishidwa kumiliki na akaitelekeza


ASKARI  wa jeshi la polisi  F  228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki
dunia mara baada ya kupigwa risasi na jambazi sugu mjini hapa ambapo
pia katika tukio hilo Mrakibu wa polisi katika wilya ya Arusha
Vijijini Bw  Faustine Mwafele naye alijeruliwa na risasi.

Kwa mujibu wa Kamanda  wa polisi mkoa wa Arusha  Thobias Andengenye
alisema kuwa tukio hilo lilitokea January tatu mwaka huu  majira ya
saa kumi za  alfajiri katika eneo la Shangarai  barabara ya Dispointi
wilayani Arumeru..

Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo ambapo polisi walikwenda
kufanya msako wa ghafla katika nyumba ya Bi Agness Silas na ndipo
Jambazi mmoja liyefahamika kwa jina la Hendry Samson Kaunda
alipowawahi askari hao na kisha kuwafyatulia risasi kwa mfulululizo.



Aliendelea kudai kuwa baada ya kuwafyatulia risasi hizo kwa haraka
sana na ndipo ilimpompiga Constebo  Kijanda katika eneo la shingo na
hatimaye kufariki  dunia hapo hapo, huku  Mrakibu wa polisi wa wilaya
ya Arusha vijijini naye alijeruliwa begani hali ambayo ilimsababishia
maumivu makali sana.


Aidha alisema kuwa mara baada ya jambazi huyo kufanikisha kuua pamoja
na kujerui alitoroka katika eneo hilo la tukio pamoja na mwenye nyumba
hiyo ambaye ni bi Agness Silas na kukimbia mahali pasipojulikana mpaka
sasa.
“huyu jambazi anahisiwa kufanya matukio mbalimbali ya kuua na pia
inadaiwa kuwa ametoka magereza lakini sisi bado tunaendelea na msako
mkali sana wa kuhakikisha kuwa tunamshikilia kwa kuwa watu kama hawa
ndio chanzo kikuu cha kuvunjika kwa amani "alisema  Andengenye.



Pia  alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi
waliendelea  na msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo
ilikuwa inasadikiwa kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta
vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za
ujambazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Alitaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya
Short gun ,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi
za kuvaa usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika
shuguli mbalimbali za uhalifu.

Hataivyo Bw Andengenye aliongeza kuwa mara baada ya kufanya msako
katika nyumba hiyo waliendelea na msako kwa Bi Rehema  Ally katika
kijiji cha Nambala Wilayani Arumeru  ambapo napo Jambazi mwingine
alikimbia na kasha kutupa Bunduki katika eneo la choo.

 Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto  wawili
wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao
ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye
aliyefumfungulia  mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui  askari polisi.
 
Katika hatua nyingine Kamanda Andengenye alisema kuwa bado msako
unaendelea kuhusiana na tukio hilo huku atakayefanikisha kukamatwa kwa
jambazi sugu ambaye anajulikana kwa jina la Hendy  Samson atapewa
zawadi ya milioni tano.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post