WAHIMIZA KUWEKEZA KATIKA MICHEZO

Wabunge watatu wa majimbo ya Kondoa kaskazini,Kondoa Kusini na wa viti maalum wameazimia kuweka mipango kabambe ya kuendeleza michezo na vijana ili kuwaondoa katika wimbi la kujitumbukiza kwenye starehe zaidi badala ya kuwa na mbinu halali za vipato kwa kutumia ujuzi,vipaji na nguvu zao.

Aidha akizungumza wakati wa kuhitimisha mashindano ya ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Kondoa,mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Bi,Moza Abeid Saidi amesema wao kama viongozi wa wananchi wapo tayari kuhakikisha kuwa wanapata ufumbuzi wa mahitaji ya vijana katika nyanja mbalimbali.

Aliongeza   kuwa yeye pamoja na wabunge wenzake tena akiwemo mbunge kijana mwanamichezo Juma Suleiman Nkamia watakaa pamoja na kuona mbinu zipi zitumike kuhakikisha kuwa yale yanayowakabili vijana katika kujiajiri likiwemo suala la changamoto michezoni yanatatuliwa kwa njia moja ama nyingine.

Alibainisha  kuwa yeye binafsi katika kuwasiliana na watu mbalimbali ambao ni wadau wakubwa wa michezo kutoka wilayani Kondoa wamemhakikishia kuwa wapo tayari kushiriki katika kuendeleza michezo isipokuwa tu wakishirikishwa katika hatua zote.

Kwa upande wake mchezaji mkongwe wa siku nyingi Mohamed Roshi alilalamikia tabia ya vijana wa sasa kutokuwa makini katika michezo na wavivu kwani wamekuwa wakilalamika ovyo na kutoa lugha za matusi uwanjani kila mwamuzi anapoamua jambo.

Alitoa taadhari kuwa kama tabia hiyo itaendelea maendeleo ya soka wilayani Kondoa yatakuwa magumu sana kwani vijana wadogo tu sasa hawataki hata kuwaheshimu wakubwa wao wanapowakosoa na kuwaona kama wanawasumbua tu.

Aliwaasa wafanye mazoezi kwa nguvu na kuacha starehe kama vile uvutaji na unywaji wa pombe kali huku wakizembea mazoezi kwani wataonekana wazee kuliko hata waliowatangulia katika masuala ya michezo tangu zamani.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post