ikionyesha wachezaji wa timu ya Jkt Oljoro wakiwa na mwalimu wao Ally Mohamed(kidi) wakimsikiliza mkuu wamkoa wakati alipowatembelea katika uwanja wa sherkh Amri Abeid
katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Adam Broun Akimsomea mkuu wa mkoa historia fupi ya chama cha mpira mkoa
mkuu wa mkoa wa arusha akiwa anaongea na wachezaji wa timu
ya Jkt Oljoro jana wakati alipokuja kuongea na akiongoza na baadhi ya
wadau wa soka mkoani Arusha
ikionyesha mmoja wa wadau wa soka wa mkoa wa arusha Aliejulikana kama
Huseni gonga akiwa anawapa nasaa wacheza wa timu ya
Jkt Oljoro kabla ya kuondoka
mmoja wa wadau wa mpira aliyejulikana kwa jina la Dalia akikabidhi shilingi milioni mbili kwa ajili ya timu ya Jkt Oljoro kwa meneja wa timu hiyo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa akikabidhi hundi ya milini tano kwa muheka azina wa timu ya Jkt Oljoro
Jumla ya shilingi milioni 15 pamoja na jezi mbili na mipira
mitano zimetolewa na wafanyabiashara mbalimbali wa mkoa wa Arusha kwa ajili ya
kuisaidia timu ya Jkt Oljoro ambayo inashiriki katika mzunguko wa pili wa ligi
kuu ya vodacom Tanzania.
Wafanya biashara hao ambao ni wadau waliongozwa na mkuu wa
mkoa wa Arusha walichangia fedha hizo kwa ajali ya kusaidia timu hiyo ambayo ni
timu pekee ya mkoani hapa inayoshiriki ligi kuu.
Akiongea wakati wa kukabidhi fedha hizo mkuu wa mkoa wa
Arusha Mulongo Magesa alisema kuwa wameamua kuchangia timu hiyo kwakuwa ni timu
pekee ya mpira wa miguu ambayo
inawakilisha mkoa wa Arusha katika ligi kuu
Alibainisha kuwa amefurahishwa sana kukutana na timu hiyo kwani alivyofika hapa aliulizia kwanza
kuhusiana na michezo kwani swala hili la
michezo ata raisi ameelezea kuwa iendelezwe.
“kama mkoa kama mkoa na kiongozi wa mkoa michezo ni kipaumbelele
katika shughuli zangu zote hivyo nitaakikisha michezo inaendelea katika mkoa wa
Arusha na ifikie tuwe na timu hata nne
zilizopo ligi kuu’’alisema Mulongo
Alisema kuwa michezo ni ajira hivyo wachezaji wakienda
kuwakilisha mkoa wawakilishe vizuri
vyema mkoa kwani kwa kupitia michezo pia wanaweza wakapata ajira.
“mnapokuwa mnacheza vizuri kwa amani basi mtaweka washabiki
katika amani na upendo na kupitia michezo hii mnatakiwa kuunganisha mkoa ili
mkoa uwe mkoa wa amani hili ndio jambo la kwanza nataka mlifanye mtumie michezo
yenu kuimarisha amani ya mkoa na wananchi kwa ujumla’alisema Mulungo
Alisema kuwa iwapo watafanya hivyo itawasaidia hata wao
wenyewe katika swala zima la ajira kwani kupitia amani yao wanayoonyesha katika michezo wanaweza
kupata ajira hata heshima kwa ujumla.
Alisema kuwa yeye akiwa kama
mkuu wa mkoa atakuwa na bega kwa bega kuhakikisha hawapati shida iwapo
watacheza vizuri na kuonyesha moyo na kubainisha kuwa iwapo watafanya vizuri
zaidi watazidi kuwahamashisha wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia michezo.
Alibanisha kuwa kwakuwa timu hii ya Jkt Oljoro inasaidia
kutangaza timu ya mkoa wa Arusha hivyo wadau mbalimbali washabiki wajitokeze
kuisaidia kwa fedha na kama fedha hamna basi
japo kwa kujitokeza katika mechi zao ambazo watazicheza hapa nyumbani pamoja na
nje kwa wale ambao wataweza kwenda kuwashangilia.
Aliwataka wachezaji kujituma vilivyo ili kuweza kuendelea kuwapa moyo washabiki wa
mpira wa mkoa wa Arusha na nje ya mkoa na wasiiige mambo ya wachezaji wengine
ambao wakipata majina kidogo wanabadilika.
“unakuta mchezaji akishaandikwa mara mbilil tatu anaanza
kuvuta bangi kutoga masikio na wakati maandalizi
yale ya kutoga masiko na hayo yote bora ukafanye zoezi na mengine mengi
akiambiwa na mwalimu amsikilizi kisa kaandikwa na kutajwa kwenye radio mara
mbili tatu kitu ambacho kinawapoteza wachezaji wengi kwani jamani nyie hamuwaoni
wachezaji wa nje wanamahela mabilioni ya mahela lakini bado hawafanyi ujinga
hawaridhiki na umaarufuwanatafuta hela japo wanazo hivyo nachotaka kusema
msiige jitaidini na mfanye kitu kwa malengo hapo mtafanikiwa”aluisema Mulugo.
Mulugo aliwataka wachezaji wa timu ya Jkt Oljoro kuendelea
kuwa na nithamu ili kuweza kuendeleza mkoa pamoja na kutangaza mkoa wao na
iwapo watafanya hivyo wadau wengi watajitokeza kwa wingi kuwashika mkono na
kuwasadia kwa hali na mali.
katika kikao hicho kulikuwa na wadau wengi waliojitokeza
kuishika mkono timu hiyo wakiwemo benki ya NMB ambayo imehaidi jezi mbili
pamoja na mipira mitano na vifaa vingine vya mazoezi,mamlaka ya maji safi na
maji taka mkoa wa Arusha (AUSA)ambao
walitoa milioni moja,|Meya wa jiji la Arusha ambaye alitoa laki tano,Huseni
Gonga ambaye alitoa shilingi milioni moja.
Wengine ni Dalia ambaye alitoa milioni mbili,Papa king
ambaye alitoa shilingi milioni moja,Matiasi Manga ambaye alitoa milioni moja ,mkuu wa mkoa ambaye
ametoa milioni tano pamoja na mkoa ambao wameungana na wilaya ambao walitoa shilingi milioni nne
pamoja na mdau mengine ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja ambaye
alitoa viatu pea 30 vya wachezaji.
Pia Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejulikana kwa jina moja
la Dalia aliiaidi timu hii kuwa iwapo itafika hatua ya nusu fainali
itawazawadia kiasi cha shilingi milionil kumi kwa timu nzima.