No title


SERIKALI imesema utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya
umma haukuwa wa makosa kutokana na mafanikio makubwa yayoonekana sasa
katika maeneo yaliyowekezwa hususani kwa viwanda vya sukari.
Naibu waziri wa kazi na ajira Dk Makongoro Mahanga aliyasema hayo
baada ya kufanya ziara ya siku moja katika kiwanda cha Sukari TPC Ltd
na kuona shughuli za uzalishaji sanjari na kutembelea mashamba ya
kiwanda hicho ambapo aliridhishwa na juhudi za wawekezaji hao.
“Yapo maneno yanayotolewa na baadhi ya watu wanaosema kuwa sera ya
ubinafisishaji wa mashirika ya umma haukuwa na tija….baada ya
kutembelea kiwanda hiki,niseme sasa kuwa uwekezaji haukuwa na
makosa.”alisema Mahanga..
Dk Mahanga alisema juhudi zilizofanywa na mwekezaji wa kiwanda cha TPC
,kampuni ya Sukari(Sukari Investment Company),SIL inayomiliki hisa
asilimia 75 na serikali asilimia 25,zinaungwa mkono na serikali kwa
ujumla.
Awali afisa mtendaji mkuu wa kiwanda hicho,Robert Baisac,alimueleza
naibu waziri Dk mahanga kuwa TPC ina eneo la ardhi Hekta 16,000 lakini
eneo linalofaa kwa ajili ya kilimo cha miwa ni Hekta 8050 na eneo
lililobaki lina magadi na halifai kwa kilimo chochote.
Alisema hata hivyo pamoja na kilimo cha zao hilo kutegemea maji ya
mito na yaliyochimbwa ardhini,kiwango cha uzalishaji kinapanda kila
mwaka ambapo mwaka 2000 walizalisha tani 35,000 lakini hadi kufikia
msimu wa 2010/2011 wamefikia tani 86,000 za sukari licha ya kuwepo kwa
ukame katika miezi ya Oktoba na Novemba 2010.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post