Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anaongea katika mkutano wawaandishi wa habari na wadau
Mchungaji Andrew kajemba wa kanisa la Anglican ,St James kalolini akimwaga cheche
MCHUNGAJI
Andrew Kajembe wa kanisa la Anglican, St James kaloleni mjini hapa amewataka
wanasiasa wote ndani ya jiji la Arusha kuepukana na migogoro juu ya viti
mbalimbali vya uongozi ambavyo wao hawajavipata na walikuwa wanavitaka
kwani kwa kufanya hivyo wanachochea malumbano ambayo hayana msingi huku
umaskini nao ukizidi kuongezeka katika jamii zao.
Bw
Kajembe aliyasema hayo mapema jana wakati akifungua mkutano baina ya wadau wa
habari kwa mkoa wa Arusha pamoja na wanachama wa chama cha waandishi wa habari
mkoa wa Arusha(APC)
Alisema
kutokana na migogoro na migongano ya kisiasa imekuwa ni kikwazo mojawapo cha
kufanya Mkoa wa Arusha kushindwa kufikia hatua ambayo imekusudiwa hali ambayo
inamkandamiza mwananchi mwenye kipato cha chini ambaye kimsingi anategemea mkoa
na serikali kwa ujumla katika kutatua kero zinazoikabili jamii.
“hapa
Arusha damu imeshamwagika sana sasa nawasihi sana viongozi wote wa siasa
kuhakikisha kuwa mnaacha tofauti zenu za kisiasa na badala yake mnaangalia
maitaji muhimu kwa Mwananchi wa mkoa huu,na pia acheni tabia ya kungangania
viti vya uongozi ambavyo hamjavipata kwani kwa kufanya hivi huu sio uzalendo wa
kweli wa Mtanzania na kamwe kwenye kiti cha uongozi hamuwezi kuwa wawili bali
ni mtu mmoja pekee.”alisema Bw Kajembe.
Aliongeza
kuwa endapo kama hali ya migongano mbalimbali ndani ya uongozi kwa Mkoa
wa Arusha itakomaa ni wazi kuwa rasilimali nyingi sana zitaweza kupote hukuwanananchi nao
wataishi katika hali ya kimaskini kutokana na kukosa haki zao za msingi.
Aliwataka
wanasiasa wote kuhakikisha kuwa wanafanya kazi ambazo zimewaweka katika viti
vyao vya uongozi kwa kuwa demokrasia ndiyo iliyotumika katika chaguzi
mbalimbali, hivyo demokrasia hiyo inatakiwa kutumika hata kwa upande wa kuleta
maendeleo kwa mji huu.
Awali
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema alisema kuwa Arusha hakuna
matatizo , hususani katika suala la Meya wa jiji Bw Gaudence Lyimo bali Tatizo
lilopo ni Mchakato wa Kumpata Meya.
“naomba
niwafahamishe kuwa sisi Chadema hatumchukii Meya wa jiji ila shida yetu ipo
pale kwenye mchakato jinsi alivyopatikana kwa maana hiyo iyo ndiyo shida yetu
kubwa sana”alisema
bw Lema
Pia
alisema kuwa kwa Jimbo la Arusha mjini ili kuweza kupata uwiano mzuri katika
kuleta maendeleo ni lazima kuwe na umoja wa hali ya juu sana kwa kuwa bado
jamii nyingi sana bado zinaitaji msaada wa viongozi mbalimbali.