KATA YA LOIBORSIRET YAPATA DIWANI

Diwani wa Kata ya Endiamtu Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Lucas Zacharia akipongezwa na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa CCM Mkoa wa Manyara kwenye uchaguzi uliofanyika mjini Babati.

Diwani wa Kata ya Endiamtu Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Lucas Zacharia akipongezwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara,Dorah Mushi baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa CCM Mkoa wa Manyara mjini Babati (katikati) ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Endiamtu Issa Katuga.



Diwani wa Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Lucas Ole Mukusi amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi mjini Babati,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Pandu Amiri Kificho alisema Ole Mukusi alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 629.
Kificho alisema wagombea wengine wawili waliopitishwa kugombea nafasi hiyo walijitoa lakini walipigiwa kura ambapo Godwin Nagol Kapurwa alipata kura 19 na Issa Omary Katuga alipata kura 18.
Alisema Fratey Massay alichaguliwa kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo kwa kupata kura 41 na kuwabwaga wagombea wengine Michael Ngayda Tsaxara aliyepata kura 9 na Ernest Fiita Sulle alipata kura 2.
Alisema nafasi ya Katibu Uchumi na Fedha ya mkoa huo ilibidi irudiwe baada ya mshindi kutopata nusu ya kura kwani Lucas Zacharia alipata kura 26 Gidamon Gapchojiga kura 14,Janes Darabe kura 9 na Gabriel Bukhay kura 3.
Hata hivyo,uchaguzi huo uliporudiwa Kificho alimtangaza Diwani wa Kata ya Endiamtu,Zacharia kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa mkoa wa Manyara kwa kupata kura 34 dhidi ya Gapchojiga aliyepata kura 18.
 Aliwataja wajumbe wa wilaya wa Halmashauri Kuu ya CCM wa mkoa huo wa wilaya ya Babati mjini ni Vicky Mushi (389) na Renalda Ndekubali (383) na wilaya ya Hanang’ ni Daniel Tluway (463) na Samwel Kawanga (268).
Wilaya ya Babati Vijijini ni Mariam Kwimba (589) na Raphael Sumaye (273) Kiteto ni Sarah Losuritia (546) na Ahmed Muya (306) Simanjiro ni Awadhi Omary (360) na Paulo Sanka (301) na Mbulu ni Joseph Mandoo (353) na Aloyce Baira (169).  
Akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa mkoa huo Zacharia alisema atawatumikia wanachama wa mkoa wa Manyara hata usiku wa manane kwani yeye ameomba utumishi kwao hajaomba ubosi.
Naye,Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Ole Mukusi alisema changamoto kubwa atakayopambana nayo kwenye uongozi wake ni kuhakikisha analirudisha jimbo la Mbulu linaloshikiliwa na Chadema na kata zinazoshikiliwa na upinzani.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia