TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAMBIRAMBI MSIBA WA
WACHEZAJI RUSUMO FC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya wachezaji watano wa timu ya Rusumo
FC ya mkoani Kagera vilivyotokea jana jioni (Oktoba 16 mwaka huu).
Rusumo FC ilikuwa ikitoka kwenye
mechi ya michuano ya Polisi Jamii Wilaya ya Ngara ambapo ikiwa njiani kurudi
Rusumo kutoka mjini Ngara ilipata ajali ya gari na wachezaji watano kufariki
papo hapo.
Wachezaji wengine ambao ni majeruhi
wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Ngara ya Murugwanza huku wawili hali zao zikiwa
mbaya.
Msiba huo ni pigo kwa familia za marehemu,
klabu ya Rusumo FC, Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ngara (NDFA), Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla
nchini kutokana na mchango wa wachezaji hao katika ustawi wa mchezo huu kupitia
klabu yao.

TFF inatoa pole kwa familia za marehemu,
Rusumo FC, NDFA na KRFA na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
cha msiba huo mzito.
Kutokana na msiba huo, mechi zote za Ligi
Kuu ya Vodacom zinazochezwa leo (Oktoba 17 mwaka huu) kutakuwa na dakika moja ya
maombolezo ili kutoa heshima kwa marehemu hao. Mungu aziweke roho za marehemu
mahali pema peponi. Amina
KIM KUSHUHUDIA MECHI
ZA LIGI KUU Z’BAR
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars),
Kim Poulsen wikiendi hii ataanza ziara ya Zanzibar kuangalia Ligi Kuu ya Grand
Malta kuwania ubingwa wa Zanzibar.
Kim anatarajia kushuhudia mechi zilizopungua
tano akianzia kisiwani Pemba ambapo kati ya Oktoba 19 na 21 atashuhudiwa mechi
mbili zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Gombani. Mechi hizo ni kati ya mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Grand Malta, Super Falcon ambao watacheza na vinara wa
ligi hiyo Bandari, na baadaye mechi kati ya Duma na Bandari.
Baadaye atakwenda Unguja kwenye Uwanja wa Amaan ambapo
baadhi ya mechi alizopanga kushuhudia ni kati ya Mtende na Chipukizi, Mundu na
Jamhuri na KMKM dhidi ya Zimamoto.
About Woinde Shizza
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia