TAMASHA LA JAMBO FESTIVAL KUANZA KUTIMUA VUMBI OCTOBER 20 JIJINI ARUSHA
meneja wa mauzo na masoko MEGA TRADE
INVESTMENT Gudluck Kway ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo
Tamasha la vitu vya asili lijulikanavyo kwa jina
la Jambo festival linatarajia kuanza kutimua vumbi oktoba 20-28jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa idea afrika Augustino Namfua ambao
ni waandaaji wa tamasha kubwa la jambo festival
katika viwanja vya kijenge jijini Arusha alisema kuwa maandalizi
yote ya tamasha hilo yamekamilika na zaidi ya wadau 100 wamethibitisha
kushiriki .
Alisema kuwa tamasha hili ni la
kwanza kufanyika jijini hapa na linashirikisha vikundi mbalimbali
vya miziki ya asili pamoja , vyakula vya kiasili na ngoma.
Alisema kuwa katika
tamasha hilo kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo siku ya kwanza ambayo ni October
20 mchana kutakuwa na mdahalo wa sanaa
na utamaduni ambao utafanyikia via via,huku siku ya pili kukifanyika maonyesha
ya sanaa za mikono, siku ya tatu kutakuwa na chakula cha usiku maalumu kwa
wasanii wa sanaa za kiutamaduni ,siku ya nne kutakuwa na maonyesho ya vyakula
vya kiasili ambapo alisema kuwa kutakuwa na vyakula mbalimbali vya makabila
tofauti tofauti ambapo alisema vitauzwa
katika uwanja wa AICC kijenge.
Alisema kuwa lengo kuu la tamasha hili la jambo festival ni
pamoja na kuibua vipaji vya sanaa kwa vijana na pamoja na kuwaeleimisha vijana
jinsi ya kufanya shughuli za kijasiriamali pamoja na kujikinga na mgonjwa
mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Alitaja baadhi ya wathamini wa tamasha hili kuwa ni pamoja
na megatrade investment kupitia kinywaji chake cha k -vant gin,Coca Cola,Ujumbe
Ink,Arusha Hotel,Viavia restaurant,Mwandago investment,sundrise radio,Arusha
time,pamoja na Interlegence seccurty.
Kwa upande wa meneja meneja wa mauzo na masoko MEGA TRADE
INVESTMENT Gudluck Kwaya ambao ndio wathamini wakuu wa tamasha hili kupitia kinywaji chao cha Kvant gin alisema kuwa kampuni yao imeamua kuthamini tamasha hili kwakuwa ni tamasha linalodumisha utamaduni wetu pamoja na kuenzi vyakula vyetu asili.
INVESTMENT Gudluck Kwaya ambao ndio wathamini wakuu wa tamasha hili kupitia kinywaji chao cha Kvant gin alisema kuwa kampuni yao imeamua kuthamini tamasha hili kwakuwa ni tamasha linalodumisha utamaduni wetu pamoja na kuenzi vyakula vyetu asili.
Alisema kuwa hii sio mara ya o ya kwanzakuthamini matamasha
bali walishathamini matamasha mbalimbali
na wao kama megatrade watandelea kuthamini pamoja na kusaidi jamii kwa
ujumla kama sera yao kampuni yao inavyosema.
Aidha alihaidi kuendelea kushirikiana na jamii katika
shughuli mbalimbali za maendeleo na kusema kuwa huu sio mwisho wao wa kuthamini
tamasha hili watakuwa wanathamini kila mwaka huku akisisitiza wananchi wa mkoa
wa Arusha kujitokeza katika tamasha hilio
Baadhi ya wasanii ambao watatumbuiza katika tamasha hili ni
pamoja na kikundi cha kuinua vipaji vya vijana wanaoishi katika mazingira magumu
kijulikanacho kwa jina la S.U.A.

.jpg)
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia