TANZANIA YATENGA ASILIMIA 24 YA ENEO LAKE KWA AJILI YA UHIFADHI ENDELEVU
waziri wa maliasili na utalii Khamis kagasheki akiwa anawakaribisha wageni waliouthuria chakula cha usiku katika hotel ya kibo palace kilichoandaliwa na wizara
TANZANIA imetenga asilimia 24 ya eneo la Uhifadhi Endelevu kwakuwa nchi inatambua manufaa yatokanayo uhifadhi huo.
Hayo yalisemwa Jijini hapa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki wakati akielezea manufaa ya uhifadhi endelevu kwa Tanzania mbele ya washiriki wa ‘’Kongamano la Kwanza la Afrika kuhusu Usimamizi wa Utalii Endelevu katika Hifadhi za Taifa “ linalofanyika arusha na kuwashirikisha wadau wa utalii pamoja na mawaziri kuttoka nchi 13 Barani Afrika.
Alisema faida mojawapo ya uhifadhi endelevu ni kukuza utalii ambao unachangia asilimia 17 katika pato la taifa na asilimia 26 ya pato la fedha za kigeni.
Alisema Tanzania imejifunza na kufaidika na mambo mengi kutokana kuwa mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) tangu ilipojiunga na shirika hilo mwaka 1975. Alilishukuru shirika hilo kwa kukubali Kongamano hili, ambalo ni la kujadili hali ya baadaye ya utalii barani Afrika, lifanyike Tanzania.
Aliwakumbusha waalikwa kuwa Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, vya asili na utamaduni, vingi vikiwa ndani hifadhi, na kutoa mfano wa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba waalikwa wote kupigia kura vivutio vya Tanzania katika shindano linaloendelea la kutafuta maajabu 7 ya asili barani Afrika ambapo vivutio hivyo ni miongoni ya vile vinavyoshindanishwa.
Wakati akimshukuru, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani Dkt. Taleb Rifai, alisema kuwa alianza kuhisi kuwa Tanzania ni nchi ya utalii tangu alipokaribia kutua katika Uwanja wa Ndege wa KIA pale ambapo abiria katika ndege aliyosafiria walipojitahidi kusogea madirishani ili waweze kuuona Mlima Kilimanjaro.
Alisema yeye binafsi alifurahi kuuona mlima huo na kwa ubunifu wake, binadamu anaweza kufanya chochote bila kuleta madhara akitoa mfano wa pale kikundi cha utamaduni cha Wanne Star kilipofanya onyesho kwa kutumia moto bila kuleta madhara yoyote. Aliitumia fursa hiyo kuziasa nchi za Afrika kuendeleza hifadhi zao kiuendelevu ili ziendelee kuchangia katika kukuza utalii bila kuleta madhara.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia