UNESCO kuwaweshesha wajasiriamali jamii ya Kimasai Ngorongoro
utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan.
Wengine ni maofisa miradi kutoka UNESCO wakishuhudia.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akimwelezea Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel
Kristian Kileo (wa pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa
ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa zinazotokana na
mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za Wilaya ya Ngorongoro
utakavyotekelezwa juzi katika Kijiji cha Ololosokwan. Wengine ni maofisa
miradi kutoka UNESCO wakishuhudia.[/caption]
SHIRIKA la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini Tanzania linatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo
cha sanaa ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali wa bidhaa
zinazotokana na mifugo kwa akinamama na wasichana kutoka Kata tano za
Wilaya ya Ngorongoro kama jitihada za kuongeza kipato kwa familia za jamii
ya Wamasai.
Akitoa maelekezo ya mradi huo juzi katika Kijiji cha Ololosokwan mbele ya
Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo,
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues alisema mradi huo unatarajia kutekelezwa
kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
Bi. Rodrigues alimueleza Kileo kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa kituo
cha kisasa cha sanaa ambacho kitatumiwa na wajasiliamali wa jamii ya
Kimasai kwa ajili ya kuuza bidha zao za asili mbalimbali kwa watalii
wanaofika kutembelea vivutio anuai vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro inayozunguka vijiji hivyo.
Akifafanua zaidi juu ya mradi huo, Ofisa Mradi Utamaduni wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Rehema
Sudi alisema mradi huo utajumuisha mafunzo ya ujasiliamali juu ya
utengenezaji wa bidhaa za ngozi, pembe za ng'ombe pamoja na shanga ili
kuziongezea thamani na kuuzwa kwa watalii anuai wanaotembelea vivutio na
kukuza vipato vya familia hasa akinamama.
Bi. Sudi aliongeza kuwa kata zinazotarajia kunufaika na mafunzo na ujenzi
wa kituo hicho cha kisasa kwa ajili ya mauzo ya bidhaa hizo za asili za
Wamasai ni pamoja na Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili na
Kata ya Aoliani Magaidulu zote za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
"...Mradi huu utajumuisha akinamama na wasichana kutoka kata tano ambazo ni
Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili na Kata ya Aoliani Magaidulu,
tutawapatia mafunzo juu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana
na ngozi na pembe za ng'ombe pamoja na shanga ikiwa ni hatua ya kuziongezea
thamani kisha kuziuza kwa watalii ambao wanatembelea vivutio vya utalii
eneo hili hasa Kijiji cha Ololosokwan," alisema Ofisa Mradi Utamaduni
Unesco, Bi. Sudi.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia)
akimuonesha Katibu Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel
Kristian Kileo (wa pili kulia) kompyuta ndogo mpakato ambazo zimefungwa
katika darasa moja maalumu kwa mafunzo mbalimbali kwa watoto na wahitaji
wengine. Darasa hilo ni sehemu ya mradi wa kidijitali unaojumuisha Kliniki
ya kisasa ya matibabu
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia