Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari jamii na
Mkufunzi Bi Rose Haji Mwalimu (aliyesimama) wakati wa ufunguzi kijiji cha
Usagara, wilayani Misungwi mkoani Mwanza hivi
karibuni.
Na Modewjiblog team, Mwanza
Tabia
ya watu kukwepa kutoa ushahidi mahakamani ni sababu mojawapo ya wahalifu wa
mauaji ya albino kutotiwa hatiani na kuachiwa huru.
Hayo
yameelezwa katika warsha zilizoendeshwa mfululizo wilayani Misungwi, Kahama
na Bariadi za ushirikishwaji wa jamii katika kuzuia na kutokomeza ukatili,
unyanyasaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism)
nchini.
Wakichangia mada kuhusu changamoto zinazowakabili watu
wenye ulemavu wa ngozi, washiriki wamesema kwamba imekuwa ni kawaida kwa
watu kutokuwa tayari kutoa ushahidi mara wanapoitwa mahakamani kwa sababu
zisizokuwa na mashiko.
Sababu
hizo ni kuogopa kuuawa na wahusika na shinikizo kutoka kwa
wanafamilia.
“Mara
nyingi tumeshuhudia watu wanaoitwa mahakamani kutoa ushahidi hawaendi siku
kesi inaposikilizwa hata kama aliandikiwa na mahakama kufanya hivyo,
wengine huamua kuhama kabisa eneo analoishi kwa kukwepa lawama kutoka kwa
jamii au familia na kuogopa kuuawa baada ya kugundulika kuwa katoa
ushahidi,” alisema mmoja wa washiriki.
Kuachiwa kwa watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika na ukatili
hususan kukatwa viungo na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kumezua
mjadala mkubwa katika jamii kwamba jeshi la polisi haliwajibiki kikamilifu
au kuhisiwa kuwa na ushirikiano wa namna fulani na watuhumiwa
hao.
Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika
linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo
Seif akisisitiza jambo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu
iliyofanyika katika kijiji cha Nyakasungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
hivi karibuni.
“Mtuhumiwa anapoachiwa huru wanajamii wanaona kama polisi
imepewa rushwa kuwachia, hawaelewi kwamba wao wenyewe wameshiriki kwa
mtuhumiwa huyo kuwa huru kwa sababu hawana ujasiri wa kujitokeza mahakamani
kama walivyoweza kutoa maelezo ya awali kwa polisi,” wamedai washiriki
hao.
Tanzania imekumbwa na wimbi kubwa la ukatili dhidi ya
watu wenye ulemavu jambo ambalo limelitia doa taifa.
Kwa
mujibu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Mashambulizi
hayo ambayo yanahusishwa na matumizi ya viungo vya miili ya watu wenye
ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina yamepoteza maisha ya watu wapatao
73 wenye ulemavu huo nchini kuanzia mwaka 2000.
“Huku
kwetu imani za kishirikina zimeenea na waganga wa jadi ni wengi sana. Ni
kawaida kabisa kwa mtu wa sehemu hizi kwenda kwa mganga wa kienyeji ili
apigiwe ramli endapo kuna mtoto mgonjwa au kifo kimetokea katika kaya
badala ya kwenda kituo cha afya,” alisema Bahame Maduhu, mwenyekiti Kata ya
Nkololo wilayani Bariadi.
Maduhu
amesema kwamba watu wajanja wamechukua udhaifu wa wanajamii kutoka kanda ya
Ziwa kuamini ushirikina kiasi kwamba waganga wengine wenye tamaa za
kutajirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi wamehamia katika ukanda
huo.
Washiriki wakiandaa mpango kazi kwa ajili ya
utekelezaji ili kudhibiti ukatili dhidi ya ukatili ya watu wenye ulemavu wa
ngozi katika kijiji cha Nkololo, Kata ya Nkololo wilayani
Bariadi.
“Waganga hasa wanaotumia ramli na mapepo machafu ndio
wenye kuendesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ili kukamilisha
huduma za wateja wao ambao hutaka utajiri, kuchimba madini, uvuvi na
biashara nyingine, alieleza mwenyekiti huyo.
Kuzorota kwa hali ya usalama kwa watu wenye ulemavu wa
ngozi serikali ililazimika kuwahamishia katika vituo maalum kwa ajili ya
ulinzi.
Hata
hivyo kwa sababu za msongamano hali ya vituo hivyo imezorota kutokana na
kukosekana kwa huduma muhimu hususan za afya, chakula, mavazi na malazi
.
Vituo
hivyo ni Mitindo, Misungwi mkoani Mwanza, Buhangija mkoani Shinyanga,
Kabanga mkoani Kigoma na Shule ya Msingi Pongwe mkoani
Tanga.
Hadi
sasa ni vigumu kuelewa sababu za ukatili huo lakini kwa mujibu wa washiriki
wa warsha hizo utamaduni uliojenga imani za ushirikina zilizoota mizizi
katika jamii, elimu duni, biashara za uvuvi, uchimbaji wa madini, utapeli
uliojipenyeza katika tiba asili na unyanyapaa zimetajwa
kuwa miongoni mwa chanzo cha ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa
ngozi.
Hali
hii imelisukuma Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) kuandaa warsha nne mfululizo zilizowakusanya wanajamii 160 kutoka
vijiji 12 zenye lengo ya kubaini matatizo na kutafuta suluhisho katika
jamii kwa kuihusisha jamii yenyewe katika kupambana na ukatili dhidi ya
watu wenye ulemavu wa ngozi.
Miongoni mwa walioshirikiana na UNESCO kutoa elimu hiyo
ni wataalamu kutoka Shirika la Serikali la Haki za Binadamu (CHRAGG),
Baraza la Tiba Asili Muhimbili na shirika la kimataifa linaloshughulikia
masuala ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Under The Same Sun’
(UTSS).
Wilaya
ya Sengerema mkoani Mwanza ilitoa vijiji vitatu ambavyo ni Nyanzenda,
Nyakalilo na Nyakasungwa; Mwanza kijiji cha Luchili, Idetemya na Fela.
Wilaya ya Bariadi ilishirikisha kijiji cha Nkololo, Nkindwabiye na Gasuma
wakati Msalala ilitoa vijiji vitatu ambavyo ni Ndala, Busungo na
Chela.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili Dakta Edmund Kayombo akielezea umuhimu wa
waganga wa jadi kujisajili katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika
kijiji cha Nyakasungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu
ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia
kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye
albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa
dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mshiriki wa warsha ya ushirikishwaji jamii kudhibiti
ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi akiwasilisha mpango kazi wa
kikundi kazi.
Baadhi ya washiriki kutoka kata ya Nkololo
wakifuatilia kwa makini maelezo ya warsha ya siku tatu kuhamasisha ukatili
dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha
inayoshirikisha wanajamii kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti ukatili dhidi
ya watu wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika Usagara wilayani Misungwi mkoa
wa Mwanza.