BARAZA LAUNGA MKONO UUNDWAJI WA KAMATI YA KUCHUNGUZA MAPATO NA MATUMIZI




Na Woinde Shizza ,Kondoa
Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Vijijini Limeunga mkono kuundwa kwa kamati ya kuchunguza taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri hiyo ya mwezi wa dec baada ya kuikataa kwenye kamati ya Uchumi na Fedha sanjari na madiwani kukosa posho zao kwa miezi 11 sasa.
Akisoma kwenye baraza hilo Taarifa ya kamati ya Fedha na Uchumi mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gasper Mwenda Aliliambia kuwa kutokana na mapungufu yaliojitokeza wameonelea kuunda kamati ndogo ambayo itapitia mapato na matumizi ya mwezi December na kuirudishia kamati hiyo ambayo itawasilisha kwenye baraza hilo.
Amesema suala hilo limejitokeza baada ya kamati hiyo kuirudisha ripoti ya matumizi na fedha mara tatu ikiwa na mapungufu mbali mbali hivyo ilikuweza kujiridhisha wameunda kamati ndogo ya kulifuatilia hilo kwa kina na wakimaliza watawasilisha ripoti yao kwa kamati hiyo ambayo nayo itawasilisha kwa kwenye Baraza la madiwani.
“Ukiangalia Fedha za miezi ya Julai.ogasti,septemba mapato yamekuwa yakishuka toka million 13 hadi kumi hivyo mda huu tunaiomba kamati ndogo kulifuatilia hilo kwa kina utaona hata madiwani wamekosa posho zao kwa miezi 11 sasa” alisema Mwenda
Suala hilo ambalo diwani wa Viti maalum Asha Abdallah alisema kuwa japo limerudishwa kwenye kamati ya fedha ambayo nayo imeunda kamati ndogo ya kupitia na kujiridhisha bado changamoto ni kubwa kwani halmashauri imekuwa ikishuka kimapato mara kwa mara na inakabiliwa na ukata mkubwa.
Nae Mh.Ramadhan Bakari Akaitaka Halmashauri hiyo kujitathmini na kuimarisha mapato yao ya ndani kwani imeshindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake wanaolipwa malipo ya ndani kwa kipindi kirefu sasa.
Amehoji suala hilo akitanabaisha kuwa fedha zinazobaki kwenye mapato na matumizi ya Halmashauri mbona hazielekezwi kwenye miradi ya maendeleo kama elimu maji na Afya.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia