WATAKIWA KUWEKA MIKAKATI ENDELEVU ILI KUBORESHA AFYA ZA WANAOWAHUDUMIA
Baadhi
ya wataalamu wa afya wa Jeshi la Polisi kutoka katika vituo mbalimbali
nchini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo ambayo
ulifunguliwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna
(DCP) Charles Mkumbo kwa niaba ya IGP
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
akiwahutubia wataalamu wa afya wa Jeshi la Polisi kutoka maeneo
mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa semina iliyofanyika katika
hoteli ya SG Resort iliyopo jijini Arusha
Mgeni
rasmi wa ufunguzi wa semina kuhusiana na VVU na UKIMWI kwa wataalamu wa
vituo vya afya vya Polisi nchini Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu
Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki wa semina hiyo. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Dr. Charles Msenga na kushoto kwake (aliyevaa suti) ni
Mkurugenzi wa AIDS FREE Dr. William Nyagwa
Na Woinde Shizza,Arusha
Wataalamu wa afya wa
Jeshi la Polisi wametakiwa kujiweka tayari katika kujadili changamoto na kuibua
mikakati endelevu ili waweze kuboresha huduma za afya kwa watu wenye uhitaji,
askari pamoja na familia zao.
Hayo yamesemwa leo asubuhi
katika hoteli ya SG Resort iliyopo jijini hapa na Kamanda wa Polisi mkoa wa
Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili ya wakuu wa vituo tiba vya
Polisi Tanzania pamoja na wafanyakazi na watumishi wa JSI kuhusiana na
uboreshaji utoaji wa huduma za afya katika kukabiliana na jukumu la kupambana
na uzuiaji wa maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Alitoa wito kwa
Madaktari, Wauguzi na watumishi wengine wanaofanya kazi katika Zahanati na vituo
vya afya kuendelea kuwatambua wenye maambukizi ya VVU na UKIMWI kwa kuwapima,
kuwaanzishia dawa na kuhakikisha wote walioanza matibabu wanaendelea kutumia
dawa kwa kipindi chote cha uhai wao.
Kamanda Mkumbo
aliendelea kuwakumbusha washiriki wa mkutano huo kuendelea kuwahudumia wananchi
kwa uadilifu na utunzaji mkubwa wa siri za wateja wanaopatiwa huduma za VCT/CTC
ikiwa ni sehemu ya kiapo chao juu ya taaluma yao.
Naye Mganga mkuu wa
Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Charles Msenga, alisema kwamba lengo la semina hiyo ambayo inawezeshwa na JSI/AIDS
FREE ni kujitathmini namna ya utoaji huduma bora kwa askari, familia zao pamoja
na wananchi wengine wanaotumia vituo hivyo.
Alisema kwamba ubora wa
huduma ambao wanatoa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku ambapo wataalamu hao wa
afya wamekuwa wakihakikisha kwamba wagonjwa wote wenye matatizo wanapatiwa dawa
na walioacha dawa wanafuatiliwa na kuendelea kuhudumiwa.
Alisema vituo vyao vya Afya vimekuwa vikitoa Ushauri
Nasaha na Kupima (VTC) lakini pia kwa wagonjwa wamekuwa wakipata huduma za
Uangalizi pamoja na kupewa dawa (CTC) hali ambayo imesaidia watu wengi
kujitokeza kupima na kufahamu afya zao.
Awali akizungumza
katika Semina hiyo iliyojumuisha washiriki 50 kutoka vituo mbalimbali vya afya
vya Polisi nchini, Mkurugenzi wa AIDS FREE Dr. William Nyagwa, alisema kwamba
shirika hilo lisilo la kiserikali linataka siku za usoni UKIMWI uwe historia na
kuwataka wana semina hao kuendelea kujitoa kufanya kazi hiyo huku
akiwahakikishia kwamba wao wapo nyuma yao.
Aidha alitoa wito kwa askari
pamoja na familia zao kujitokeza kwa wingi kupata huduma kupitia vituo hivyo
vya afya kwani kwa mgonjwa itakuwa rahisi kuhudumiwa na kuwahakikishia kwamba wataalamu
wanaotoa huduma katika vituo vya afya wamekula kiapo hivyo wasiwe na wasiwasi
juu ya usiri.
Dr. Nyagwa alisema
Semina hiyo pia itatoa uhuru kwa washiriki wote kuelezea changamoto
zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili ziweze kutatuliwa.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia