WANAFUNZI 160 AMAN KARUME WILAYANI KONDOA WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA WILAYA
Na Woinde Shizza, Kondoa
Wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume ilyopo kata ya Pahi wilayani Kondoa wameandamana
hadi ofisini kwa mkuu wa wilaya hiyo Sezaria Makota wakidai kupewa Adhabu za
kuchimba visiki, na vibarua vya kushusha mizigo ya ujenzi wa shule jambo ambalo
linawakatisha masomo yao.
Hayo
yamebainika wakati mkuu huyo wa wilaya akiongea na wanafunzi hao kwenye ukumbi
wa Kondoa Irangi na kutoa Agizo la wanafunzi hao kurejea shuleni wakati
malalamiko yao yakiendelea kutatuliwa na mwisho wake ni jumamosi ya wiki hii
yote yatakuwa yameshughulikiwa.
Amesema kuwa
malalamiko waliowasilisha ofisini kwake na viongozi wa wanafunzi hao ni pamoja
na kukosa huduma sahihi za afya ikiwemo kutokuwepo kwa dawa kwenye kituo cha
Afya Pahi na kadi za CHF za wanafunzi wengine kutofanya kazi,pia kupewa Adhabu
ya kuchimba visiki wakati wa masomo.
Mkuu huyo wa
wilaya Amebainisha kuwa uonevu kwa wanafunzi hao ni marufuku ambapo akawataka
Afisa elimu kuhakikisha kunakuwepo na Box la maoni shuleni hapo sanjari na
kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa wale wote watakaokaidi Agizo hilo.
“Nawataka
watoto wangu kubwa ni nidhamu ila mwende shule wakose sababu na mbadilike kwani
watawatafutia sababu ila malalamiko yenu mpaka jumamosi mabadiliko mtayaona na
tunaendelea kuyafuatilia kwa ukaribu nami ntafika shuleni hapo wakati wowote
wiki hii” alisema dc
Miongoni mwa
malalamiko ya wanafunzi hao ni matibabu hafifi,kadi za CHF hazifanyikazi,kupewa
adhabu za kuchimba visiki wakati wa masomo, kulipia Nembo ya shule hadi sasa
hawajapewa, makamu wa mkuu wa shule kumpiga mwanafunzi teke na michango
iliyopitiliza ikiwemo kutakiwa kulipia rimu 8 kwa ajili ya majaribio na
mitihani.
Amesma
kuwawaraka wao ameoupokea na atahakikisha anaufanyiakazi haraka iwezekanavyo na
kumuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Vijijini kuhakikisha
wanafunzi wote waliofika ofisini kwake na wale 7 walioshindwa kufika ofisini
kwake wanafika salama shuleni na wasibugudhiwe na waendelee na masomo yao.
DC Makota
amewataka waalimu wote ambao hawaingii Darasani kuingia mara moja
kufundisha,huku akisema kuwa wanafunzi hao ni marufuku kufanya vibarua vya
kubeba mizigo ya ujenzi wa majengo na kumtaka pia mkurugenzi kuhakikisha
wanafunzi saba waliobakia njia kama wapo salama
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia