WATANZANIA WATAKIWA KUMLILIA MUNGU KILA MMOJA NA IMANI YAKE

askofu mkuu wa kanisa la Gombo la chuo lililopo ndani ya mji mdogo wa Ngaramtoni uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Daniel Methew alipokuwa akiongea katika matukio ya kusimikwa kwakwe kuwa askofu 


 Na Woinde Shizza , ARUSHA 


Kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi linayopelekea kuwepo kwa hali ya ukame kila mtanzania ametakiwa kufunga na kumuomba Mungu kwa imani yake ili aweze kuondoa hali hii na kuleta mvua .


Hayo yamebainishwa na askofu mkuu wa kanisa la Gombo la chuo lililopo ndani ya mji mdogo wa Ngaramtoni uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Daniel Methew alipokuwa akiongea katika matukio ya kusimikwa kwakwe kuwa askofu ,kuzindua kanisa pamoja na uzinduzi wa kitabu chake kijulikanacho Kwa jina la nguvu ya ukombozi ambapo alisema kuwa kutokana na hali ya ukame iliopo Sasa ni vyema Kila mtanzania akaomba Kwa dini yake ili hali ibadilike


Alisema kuwa japo kuwa wataalamu wanasema kuwa hali hii imetokana na uharibifu wa mazingira uliofanywa na wananchi wenyewe Kwa kukata miti ovyo kunasababisha tusipate mvua Kwa wakati.


"Naweza kusema Kuna mambo mawili kwanza uharibifu wa mazingira unaweza kutusababisha tusipate mvua kwa wakati lakini jambo kingine maovu yetu ,maandiko yanasema ikiwa watu wangu walioitwa Kwa jina langu wataomba watalia Mungu atawasikia na ataiponya nchi " Daniel


Alisema ni vyema watanzania tukamtafuta Mungu ili atukumbuke na mvua kwa sababu mifugo inaangamia na watu wanakufa na njaa Kwa sababu atujapata mvua kwa muda mrefu.


Aidha aliwataka wananchi kuendelea kumuombea Rais wa Tanzania Samia Suluhu kwakuwa amekuwa kiongozi msikivu na ambaye anawajali wananchi wake bila kujali itikadi ya vyama vyao pia amekuwa ni kiongozi wa kuwatia moyo wachungaji .


Aliwataka watanzania kuendelea kuendeleza umoja na mshukamano uliokuwepo katika nchi yetu ili amani ya nchi iendelee kuwepo. 



Kwa upande mchungaji wa kanisa hilo pasta Pendo kileo alisema kuwa ni vyema Kila mtanzania akakaa kwenye mikono ya bwana ili Mungu aviruhusu vile ambavyo amevitengeneza na kuviweka duniani tuvipokee na kuviishi .


Aidha aliwataka watanzania kuinuka kushikamani ili kuweza kuijenga nchi yetu ,waweze kuwa na nia na sauti moja ili kuweza kuijenga nchi ya Tanzania na wakiamua watafika mbali.



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post