Kuna dhana nyingi potofu hususan kuhusu uvaaji wa ‘sidiria’ . Wakati mwingine inaweza kukanganya usipojua ni upi ukweli na upi ni uongo kuhusiana na hili.
Sidiria huwasaidia wanawake kuvaa nguo zao vyema . Wasichhana huvaa sidiria kuanzia wanapokuwa shule na kuendelea . Wavaaji wapya wa sidiria huwa na wasi wasi usioelezeka kuhusi
ana nazo.
Baadhi ya watu huamini kuwa kuvaa sidiria kunaweza kusababisha saratani ya matiti. Kuna wanawake wengi ambao huwa hawahisi kuwa na starehe wavaapo sidiria.
Wengine huwa na mashaka kuwa wanapovaa sidiria , kutakuwa na mabadiliko katika muundo wa mwili wao, na kwamba matiti yao yatalegea.
Lakini je kuvaa sidiria au kutoivaa kunabadilisha kweli mwili wa mwanamke? Ni nini ambacho wanawake wanafaa kukijua kuhusu matiti yao ? Na madaktari wanasema nini?
'Matiti yanafaa kueleweka'
Daktari bingwa wa uzazi wa wanawake Gynecologist Balakumari sanasema kwamba wanawake wanafaa kuelewa miili yao na wanafaa kuyaelewa matiti yao.
"Matiti ya mwanamke yameundwa na tishu ambazo zina mafuta na tezi za mamalia. Kama zilivyo tezi katika kinywa kwa ajili ya kutengeneza mate, matiti pia yana tezi za kutoa maziwa.
Baadhi ya watu wanatezi zaidi za mamalia na kiwango cha chini cha mafuta . Inategemea kulingana na muundo wa mwili wa kila mtu.
Tezi za mamalia husinyaa kadri umri unavyokwenda. Ni jambo la kawaida kwa matiti kusinyaa, sio kwamba kuvaa sidiria kutayafanya yawe makubwa ," anafafanua.
Pia ni Imani kuwa kufaa sidiria inayobana kunaweza kusababisha saratani, alisema.
"Iwapo nguo ya ndani inabana sana mwili, kunaweza kuwa tatizo la Ngozi. Upepo na jasho vinaweza kusababisha muwasho na ushumbufu.
Kuvaa sidiria ambayo inabana sana kunaweza kusababisha maumivu ya matiti. Ni muhimu kuchagua sidiria yenye ukubwa unaofaa. Hakuna haja ya kuhofia saratani ya matiti kwasababu hii , alisema.
"kwa wanawake wenye matiti makubwa, ni jambo la kawaida kwao kuinama. Hii inaweza kusababisha maumivu ya mgongo.
Maumivu ya mgongo yanaweza kuepukika iwapo sidiria itavaliwa kwa usahihi .
Wanawake wanafaa kuelewa kwamba wanafaa kuvaa sidiria – kwa muda mfupi . Usiendelee kuivaa kama utahisi inakukosesha raha. Hakuna hatari kwa hilo.
Hakua ubaya au uzuri wa kuvaa sidiria kama haikubani na kukukosesha raha . Haina athari yoyote kwa matiti," anasema Dkt Balakumari.
Je kuna dawa za kuzuia kusinyaa kwa matiti?
Dkt Kavya Krishnan wanataka wanawake waelewe kwamba kusinyaa na kuanguka kwa matiti ni jambo la asilia la kimaumbile na ni mchakato wa kawaida kwa mwanamke.
"Si wanawake pekee, wanaume pia wanahitaji kuwa na uelewa kuhusu hili. Matarajio ya ya wanaume kwa miili ya wanawake ndio yanayowafanya baadhi ya wanawake kukosa raha na kuchoka ," alisema.
"Kuna aina mbali mbali za krimu kwenye intaneti . Yote ni udanganyifu. Krimu bila shaka hazizuii matiti kusinyaa. Hakuna ushahidi wa kimatibabu kuhusu hili.
Watu hawapaswi kudanganywa na aina hizo za matangazo ya kibiashara. Watu wanafaa kuwa na akili ya kutosha ya kutokubali kufanywa wajinga na aina hizo za matangazo ya biashara. Mtu anafaa kuwa mwelevu wa kutosha kukubali mabadiliko asilia ya mwili.
Ni jambo la kawaida kwa wanawake kushuhudia matiti yao yakianguka kadri umri unavyoongezeka. Wanawake wanaonyonyesha matiti yao hulegea. Hiki ni kitu kinachowapata wanawake wote duniani. Hakuna anayeweza kuepuka hali hii, kwahivyo hakuna sababu ya kuwa na wasi wasi kuhusu hili.
Pia kuna Imani potofu kuwa kunyonyesha husababisha matiti ya mwanamke kusinyaa. Lakini hili sio kweli. ‘’Hakuna madhara yanayosababishwa na mwanamke kunyonyesha ," anaeleza.
Je kama una matiti madogo?
Dkt Balakumari sanasema baadhi ya wanawake wenye matiti madogo huwa wanahisi kutojiamini, lakini hili sio suala la kukutia wasiwasi.
"kila mtu ana aina tofauti ya maumbile ya mwili . Hakuna kitu kama umbo lisilo na kasoro, iwapo utafurahia maumbile ya mwili wako mwili wako na matiti yako ya asilia.
Kwa mfano, wanawake wney matiti makubwa wanaweza kupata maumivu ya mgongo au mabega. Wenye tatizo hilo wanaweza kufanyiwa upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti. Upasuaji huu huitwa ‘’upasuaji wa kupunguza matiti'.
Sawia na wale wenye matiti madogo wanaweza kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti kama watataka kufanya hivyo
Uchunguzi wa kibinafsi baada ya hedhi
Dkt Manu anasema wanapaswa kujichunguza binafsi nyumbani mara moja kila mwezi ili kujilinda wao wenyewe na saratani ya matiti .
“Kila mwezi baada ya hedhi, wanawake wanapaswa kuchunguza matiti yao. Chunguza matiti yako taratibu ukiyakanda kwa viganja vyako. Iwapo utahisi kitu tofauti au uvimbe, pata ushahuri wa daktari mara moja. Hasa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30 wanapaswa kufaya uchunguzi huu kila mwezi..
Wakati wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 40 wanafaa kufanyiwa uchunguzi wa kipimo cha mammogram mara moja moja. Dalili zozote za saratani zinafaa kutibiwa mara moja .
Ni muhimu kwa wanawake kupatia kipaumbele afya yao, kwasababu wanaweza kuepuka matatizo mengi," alisema.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia