Na Rose Jackson ,Arusha
Wakazi wa loliondo na ngorongoro wamesema kuwa tiba pekee ambayo itawasaidia wafugaji wa maeneo hayo ni upatikanaji wa katiba mpya ili iweze kubadilisha mfumo uliopo.
Wameyasema hayo katika kumbukizi ya mwaka mmoja ya mateso waliyopitia wananchi wa loliondo na ngorongoro ambapo wamesema kuwa namna pekee ya kuondokana na adha wanayopitia wafugaji ni upatikanaji wa katiba mpya.
baadhi ya wananchi hao akiwemo diwani wa kata ya Nainokanoka edwadr maura na mwenyekiti wa viongozi wa mila ngorongoro anaeleza kuhusiana na umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya kwa wafugaji hao
"Wafugaji nchini tunapitia wakati mgumu sana haswa loliondo maa baada ya ardhi yetu kuchukulikuwa na hii hali sisi inatuathiri sana ila kitu ambacho kitatusaidia ni katiba mpya kwani itatusaidia kuainisha ardhi yetu ambayo inatufanya tukose maeneo ya kulishia mifugo."alisema Maura
Aliongeza kuwa licha ya serikali kuwawekea wananchi wa loliondo na ngorongoro kikwazo lakini kamwe hawataweza kuhamia Msomera mkoani Tanga.
Nae diwani wa viti maalum tarafa ya sale kjooli kakei ameishauri serikali kuwaona wananchi wa loliondo ni wananchi na ni wahifadhi hivyo ni vema ikasitisha unyanyasaji uliopo kwani kuna huduma za afya zimesitoshwa na hivyo kulazimika kutembea umbali mrefu.
"Kwa sasa kuna huduma ambazo serikali imesitisha kwenye tarafa zote na hii inatupa changamoto hivyo mie naona serikali tukae kwa pamoja tuzungumze ili tupate muafaka kwani sisi hatuna mpango wa kwenda msomera "aliongeza diwani.
Wakazi hao wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto lukuki mara baada ya serikali kusitisha baadhi ya huduma muhimu huku watoto wa kiume nao wakiwa wanakimbilia nchini kenya kutafuta maisha na hivyo kuiomba serikali kuangalia swala hilo kwa jicho la pili.