UJIO WA SAMIA KUISIMAMISHA ARUSHA WANANCHI WAMSUBIRI KWA MAPOKEZI YA KISHINDO

 



Na Woinde Shizza, Arusha

Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, amewataka wananchi wa Arusha kujiandaa kwa mapokezi makubwa ya mgombea urais kupitia chama hicho, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa maandalizi yote yamekamilika na yatakuwa ya kipekee na ya kihistoria.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Soko Namba 68 la Kilombero, mbele ya wajasiriamali wadogo wa mboga, matunda na bidhaa mbalimbali, Ramsey alisema Samia anatarajiwa kuwasili mkoani Oktoba 1. Alifafanua kuwa mgombea huyo atasimama Usa River, wilayani Arumeru, kumsalimia wananchi kabla ya kuelekea kupumzika na kujiandaa na mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Oktoba 2 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Tutafanya mapokezi ya kishindo na tutawafundisha mikoa mingine namna mgombea urais anavyopokelewa. Kwa namna tunavyopanga mapokezi haya, hakuna mkoa wowote ambao umefanya au utaweza kufanya mapokezi kama haya. Arusha tutakuwa mfano wa kuigwa,” alisema.

Katika hatua nyingine, Ramsey aliwataka kina mama wa soko hilo kuunda vikundi ili kunufaika na mikopo ya halmashauri, akisisitiza kuwa ni fursa ya kuinua mitaji na kukuza biashara ndogo ndogo.

Aidha, alimuelekeza mgombea udiwani wa Kata ya Levolosi kuhakikisha endapo atapewa ridhaa na wananchi, anasimamia ipasavyo upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali, pamoja na kutoa elimu na matangazo kuhusu namna ya mikopo hiyo inavyotolewa.

Kwa upande wake, mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo, Salome Mollel maarufu kama mama mandongamtu kazi, alisema wanawake wa Arusha wako tayari kumpokea mgombea urais huyo kwa furaha kubwa. Alimshukuru Rais Samia kwa kuwajengea soko hilo lililowezesha kujipatia kipato na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.

“Tunamkaribisha kwa mikono miwili. Huu ni wakati wa wanawake na wananchi wote kuonyesha mshikamano wetu. Tutajitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu kumkaribisha kiongozi wetu,” alisema.



Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey, amewataka wananchi wa Arusha kujiandaa kwa mapokezi makubwa ya mgombea urais kupitia chama hicho, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa maandalizi yote yamekamilika na yatakuwa ya kipekee na ya kihistoria.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia