MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha, imemwachia huru aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Arusha mjini Gervas Mgonja baada ya mahakama kudhibitisha kutokuwa na kesi ya kujibu iliyokuwa ikimkabili mahakamani hapo.
Akitoa maamuzi madogo (Rulling) mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa
mahakama kuu, Judith Kamala kwa kushirikiana na Mwendesha mashtaka wa
serikali ,Haruna Matagane alisema kuwa ,mahakama imeamua kumwachia huru
mshtakiwa huyo na wenzake wawili baada ya kubaini kuwa hawana kesi ya kujibu katika shitaka la kula njama na kutenda kosa lililokuwa likiwakabili.
Mgonja alishtakiwa
na wenzake wawili akiwemo aliyekuwa katibu wa vijana wa chadema wilaya
ya Arusha ,Anold Kamnde na Frank Njau aliyekuwa katibu wa vijana kata ya
Ngarenaro kupitia chadema ,ambapo kwa pamoja mahakama imewaachia huru
baada ya kupitia upande wa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka
ambao walileta mashaidi sita .
Hakimu
Kamala alisema kuwa,washtakiwa hao watatu kwa pamoja walikuwa
wakishtakiwa na wenzao wengine watatu jumla sita kwa kosa la unyang’anyi
wa kutumia silaha ambapo upelelezi ulipokamilika ulibaini kuwa
washtakiwa watatu akiwemo Mgonja walifungliwa shitaka hilo
la unyang’anyi wa kutumia silaha kimakosa na hivyo mahakama kuwaondoa
katika shitaka hilo na kubakia na washatakiwa watatu ambao wanaendelea
na kesi hiyo.
Washtakiwa waliobakia na kesi hiyo ya unyan’ganyi wa kutumia silaha baada ya mahakama kudhibitisha kuwa Mgonja na wenzake wawili walifungulia shitaka hilo kimakosa ni Frank Ismail, Philemon Inyasi, na Charles George.
Aidha kufuatia kesi hiyo ya unyang’anyi wa kutumia silaha iliwapelekea
mgonjwa na wenzake kukaa ndani kwa siku 120 tangu walipofunguliwa
shitaka agosti 20 hadi upelelezi ulipokamilika ,januari 15 ,2012 na kuwaondoa katika kesi hiyo na kusomewa shitaka jipya la kula njama ya kutenda kosa na kupewa dhamana. .
Ambapo kesi hiyo mpya ilianza kusikilizwa januari 15 mwaka huu , huku upande wa mashtaka ukileta mashaidi 6 ambapo kesi ilirindima kwa kipindi cha miezi kumi ndipo maamuzi maamuzi madogo ya mahakama yalipotolewa kuwa mshatakiwa hana shitaka la kujibu.
‘Kutokana na kusikiliza upande wa mashahidi kwa makini nimetosheka na ushahidi uliotolewa na mahakama na nimemwachia huru Gervas Mgonja na wenzake wawili na kuwa hawana kesi ya kujibu ‘alisema Kamala.
Akizungumza
mara baada ya maamuzi hayo ,Gervas Mgonja alisema kuwa, anamshukuru
Mungu sana kwani haki imeweza kutendeka na leo hii ameachiwa huru ,
pamoja na kuwa kesi zote hizo alibambikiziwa .
‘Kwa kweli sijui hata niseme nini namshukuru Mungu kwa kunitetea na kesi yangu imeisha na leo hii nipo huru , kwa kweli sina cha kusema ila nawaomba polisi wawe makini kabla ya kuchukua hatua, wafanye uchunguzi ili waweze kuwatendea haki sawa raia wote.
Alitoa wito kwa jeshi
la polisi kuwa makini katika utendaji wake ili kuepuka uonevu mkubwa
unaofanyika kwa kuwafungulia watu kesi ambazo hawakuhusika kitendo
kilichompelekea kukaa ndani miezi 5 bila kosa lolote na
baadaye ndipo alipogundulika kuwa alifunguliwa shitaka hilo kimakosa na
hiyo ni kutokana na kutokuwa makini kwa jeshi hilo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia