BREAKING NEWS

Tuesday, May 8, 2012

AJINYONGA KWA WAYA WASIMU

MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Maliaki Reuibern(77) mkazi wa Elkoriti amefariki dunia mara baada ya kujinyonga kwakutumia waya wa simu.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akili mpwa pwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea May tano mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi cha elkloriti kilichopo katika kata ya Moivo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa kabla ya kifo chake marehemu muda wa saa 12:00 asubuhi ndugu yake Maliaki ambaye kwa sasa ni marehumu aliamka na kumtuma mjukuu wake aitwaye Doreen Reubern dukani ili akanunue mkate na mara baada ya mkate ule kuletwa mke wake aitwae endeshi Makiaki (64)alimuandalia chai.
Alibainisha kuwa mara baada ya kumandalia chai marehemu alikunywa na marabaada ya kumaliza aliingia chumbani kwake ambapo alichukuwa waya wa simu na kujinyonga ,mara baada ya ukimwa wa muda mrefun ndipo mke wamarehemu alimtuma mjukuu wake ili akatoe vyombo sebuleni lakini alivyofika sebuleni hakumkuta babu yake ndipo .
Mpwapwa alibainisha kuwa kufuatia tukio hilo mke wa merehemu aliamua kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi na baadhi ya askari walikwenda katika eneo la tukio ambapo walichukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali ya mkoa ya maunti meru kwa ajili ya uchunguzi wa daktari na jeshi lapolisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio hilo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates