mkuu wa wilaya ya Arusha john Mongela akiwa anaapa mbele ya mkuu wa wilaya hivi leo
Mkuu wa wilaya ya Arusha akiweka saini mara baada ya kuapa
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Manasa akiwa anakula kiapo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru akiwa anaweka saini ya kiapo mara baada yakumala kuapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha magessa Mulongo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akiwa anapokea zawadi ya maua kutoka mmoja wa mfanyakazi kutoka ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha
Mkuu mpya wa wilaya ya Karatu Daudi Mtibenda akiwa anasaini mara baada ya kuapa mbele ya mkuu wa mkoa
wakuu wa wilaya wa mkoa wa Arusha wakiwa wamekaa kwa pamoja mara baada ya kula viapo wakisikiliza hutuba kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Arusha hivi leo
mkuu wa mkoa wa Arusha katika kati Magesa Mulongo akiwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha aliowaapisha
Baadhi ya wabunge wa majimbo ya mkoa wa Arusha waliuthuria pia
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ameyataka mabaraza
yote ya madiwani wa mkoa wa Arusha kupitia upya ripoti za mkaguzi mkuu wa
Serikali (CAG) na kuhakikisha kuwa inawachukulia hatrua kali za kisheria
watumishi wote ambao ndio chanzo cha hati chafu
magesa aliyasema hayo wakati akion wakuugea na waandishi wa habari mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya wapya wa wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha mapema
Alisema kuwa kamwe mkoa wa Arusha haiutaweza kuvumilia
utendaji mbovu wa watumishi ambao kila mara wanachangia kwa kiwango cha hali ya
juu kukithiri kwa hati chafu wakati hakuna vyanzo vyovyote vile ambavyo
vinasababishia halmashauri kuwepo kwa hati chafu
Alibainisha kuwa ili kukomesha tabia hiyo madiwani wote
wanatakiwa kukagua ripoti zote na kutokana na hali hiyo hawapswi kuwa na uoga
au huruma kwa kuwa hali hiyo ndiyo chanzo kikubwa sana hata cha umaskini.
“leo naawapiusha wakuu wa wilaya na pia napenda kuwataarifu
kuwa hakikisheni kuwa kuanzia sasa mnaungana
na madiwani kukagua ripoti hiyo kwa kuwa halmashauri zote zimepata hati
chafu kasoro halmashuri ya Meru pekee”alisema Mulongo
Mbali na hayo alisema kuwa katika halmashuri zote za mkoa wa
Arusha kasoro ya Meru kuna mambo makubwa sana
ambayo yanaendelea lakini kupitia msaada wa wakuu wapya wa wilaya zote wataweza
kusaidia halmashauri hizo.
Bw Mulongo alibainisha kuwa wakuu hao wapya wa wilaya
hawapswi kuangalia hekima ya kiongozi ambaye hana maadili na badala yake
wanatakiwa kufuata sheria za Nchi kwa kuwa mara nyingine huruma ndiyo
inayochangia sana
hati chafu
Awali aliwataka wakuu hao wapya wa wilaya kuhakikisha kuwa
wanafuatilia masuala mbalimbali ya kijamii hasa pale kwa serikali za vijiji
ambazo zinakabiliwa na changamoto kubwa sana
Mulongo alifafanua kuwa kupitia msaada wa wakuu hao wapya
wa wilaya wataweza kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto
ya ugumu wa kazi ambao unasababisha watendaji wa vijiji mara nyingi
kulazimishwa na wananchi kujiuzulu wakati wapo sawa kwa mujibu wa sheria
Hataivyo katika zoezi hilo
wakuu wapya wa wilaya sita za mkoa wa Arusha waliapishwa tayari kwa kuanza kazi
za kuwasaidia wananchi katika shida mbalimbali
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia