BREAKING NEWS

Thursday, May 10, 2012

KIKRAIS KIKWETE ATANGAZA WAKUU WAPYA WA WILAYA

RAIS JAKAYA KIKWETE amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwateua wapya 70, kuwabakiza kazini 63, kuwastaafisha 51, na kuwabadilisha vituo vya kazi baadhi yao.
Akitangaza uteuzi huo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kutokana na mabadiliko hayo, Wakuu wa wilaya 51 kati ya 114 waliokuwepo zamani wameachwa kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za ki-afya na umri mkubwa.
“Zamani tulikuwa na wilaya 114 na baada ya Mhe. Raisi Kikwete kuridhia kuanzishwa kwa wilaya mpya 19, hivi sasa zimefikia wilaya 133. Kwa hiyo, tumebakiza Wakuu wa Wilaya 63 na ukiongeza hawa wapya 70 unapata jumla yao ni 133,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema miongoni mwa wakuu hao wapya wa wilaya, wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 30 hadi 45 na kwamba idadi yao inafikia 40. Alisema vilevile, idadi ya wakuu wa wilaya wanawake ni 43 sawa na asilimia 32.3.
Alisema wakuu wa wilaya watano kati ya 70 wapya walioteuliwa, wametokana na wabunge wa viti maalum. “Lengo letu ni kutaka kuandaa viongozi wapya wa baadaye kutokana na kundi hili,” alisema.
Alisema Wakuu hao wapya wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ili waapishwe na Wakuu wa Mikoa husika na kisha watatakiwa kuhudhuria mafunzo maalum ambayo yatafanyika Dodoma. “Tumeandaa mafunzo hayo maalumu kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa… siyo semina bali ni mafunzo na itabidi wapewe mitihani,” alifafanua.
Orodha kamili ya wakuu wa wilaya wapya na vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:

NA.
JINA
KITUO CHA KAZI
1.
Novatus Makunga
Hai
2.
Mboni M. Mgaza
Mkinga
3.
Hanifa M. Selungu
Sikonge
4.
Christine S. Mndeme
Hanang
5.
Shaibu I. Ndemanga
Mwanga
6.
Chrispin T. Meela
Rungwe
7.
Dr. Nasoro Ali Hamidi
Lindi
8.
Farida S. Mgomi
Masasi
9.
Jeremba D. Munasa
Arumeru
10.
Majid Hemed Mwanga
Lushoto
11
Mrisho Gambo
Korogwe
12.
Elias C. J. Tarimo
Kilosa
13.
Alfred E. Msovella
Kiteto
14.
Dkt. Leticia M. Warioba
Iringa
15.
Dkt. Michael Yunia Kadeghe
Mbozi
16.
Mrs. Karen Yunus
Sengerema
17.
Hassan E. Masala
Kilombero
18.
Bituni A. Msangi
Nzega
19.
Ephraem Mfingi Mmbaga
Liwale
20.
Antony J. Mtaka
Mvomero
21.
Herman Clement Kapufi
Same
22.
Magareth Esther Malenga
Kyela
23.
Chande Bakari Nalicho
Tunduru
24.
Fatuma H. Toufiq
Manyoni
25.
Seleman Liwowa
Kilindi
26.
Josephine R. Matiro
Makete
27.
Gerald J. Guninita
Kilolo
28.
Senyi S. Ngaga
Mbinga
29.
Mary Tesha
Ukerewe
30.
Rodrick Mpogolo
Chato
31.
Christopher Magala
Newala
32.
Paza T. Mwamlima
Mpanda
33.
Richard Mbeho
Biharamulo
34.
Jacqueline Liana
Magu
35.
Joshua Mirumbe
Bunda
36.
Constantine J. Kanyasu
Ngara
37.
Yahya E. Nawanda

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates