WAZIRI WA ZAMANI WA RWANDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA
Mahakama
ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imemtia hatiani
Waziri wa zamani wa Vijana wa Rwanda, Callixte Nzabonimana kwa mashitaka
manne ya mauaji ya kimbari na kumhukumu kifungo cha maisha jela.
Jaji
Solomy Balungi Bossa kutoka Uganda aliyekuwa anaongoza jopo la majajai
watatu katika kesi hiyo amesema mahakama yake imekubaliana kwa kauli
moja kumtia hatiani Nzabonimana kwa mashitaka ya mauaji ya kimbari,
uchochezi wa mauaji hayo, kuteketeza kizazi na kula njama za kufanya
mauaji hayo katika mkoa wake wa Gitarama, katikati ya Rwanda, mwaka
1994.
‘’Kwa
uhalifu huu, na kwa mazingira yote muhimu katika kesi hii, Mahakama
inakuhukumu wewe adhabu ya kifungo cha maisha jela,’’ alitamka Jaji
Bossa huku Nzabonimana mwenyewe akiwa amesimama.
Mahakama
ilibaini kwamba Aprili 18, 1994 katika mkutano kwenye ofisi za mkoa wa
Gitarama alikubaliana na viongozi wenzake wa serikali ya mpito kuchocheo
mauaji dhidi ya Watutsi.
Katika
hukumu hiyo Nzabonimana alitiwa hatiani pia kwa mauaji ya kimbari
yaliyofanyika dhidi ya Watutsi waliokuwa wanapata hifadhi katika ofisi
za mkoa wa Gitarama.
Wakili
wa Nzabonimana,Vincent Courcelle-Labrousse aliiambia Hirondelle muda
mfupi baada ya hukumu hiyo kwamba atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
‘’Bila shaka tutakata rufaa.Kesi ndiyo kwaanza inaanza kwenye rufaa,’’ alisema wakili huyo kutoka Ufaransa.
Waziri
huyo alitiwa mbaroni nchini Tanzania Februari 18, 2008 na kesi yake
ilianza Novemba 9, 2009 na kuhitimishwa Septemba 12,2011. Mwendesha
mashitaka aliita mashahidi 20 wakati upande wa utetezi uliita mashahidi
38.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia