CHAMA cha wafanyabiashara na wanunuzi
wakubwa wa madini mkoani Arusha (TAMIDA ),wameilalamikia serikali kwa kuendelea
kuwakumbatia wawekezaji wa madini ambao ni raia wa kigeni kuendelea kufanya
biashara hapa nchini,kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kutumia leseni moja
kwa wawekezaji zaidi ya watano .
Wakizungumza na
waandishi wa habari katika kikao cha dharura kilichofanyika mjini
hapa,wafanyabiashara Augustino Kimweri na Elisha Yohana kwa niaba ya wenzao
wamedai kuwa, wawekezaji hao wamekuwa wakikiuka taratibu na sheria
za ununuzi wa ndani wa madini na kusababisha kero na adha kwa
wafanyabiashara wa ndani ikiwemo kusafirisha madini bila kukatwa .
Walisema kuwa
wawekezeji hao wamekuwa wakifungua kampuni mbalimbali za ununuzi wa madini hapa
nchini kwa kuwatumia wazawa ambao wengi wao ni wafanyakazi wao na kuwakatia
leseni kama wawekezaji, ambapo hufanya ununuzi wa madini kwa kuyafuata migodini
kinyume cha utaratibu wa lessen ya uwekezaji wa madini
,inayokataza mwekezaji kununua madini migodini.
Walisema hali hiyo
imekuwa ikisababisha wafanyabiashara wa ndani kukosa soko la upatikanaji wa
madini kutokana na wawekezaji hao kuyanunua kwa bei kubwa na kuyasafirisha moja
kwa moja bila hata kuyakata kama taratibu za leseni zao
zinavyoelekeza.
Aidha waliongeza
kuwa, wawekezaji wamekuwa wakisafirisha madini yenye uzito wa gramu 1 na
kuendelea ambayo serikali imepiga marufuku kuyasifirisha madini hayo kabla
hayajakatwa hapa nchini huku wakichanganya na madini yenye uzito wa gramu 0.9
ambayo serikali imeyaruhusu yasafirishwe bila kukatwa.
Walisema kuwa,
hali hiyo inakiuka sheria ya uwekezaji wa madini nchini ,ikiwa ni pamoja na
kukosa soko la biashara ya madini hapa nchini kwa kuwa idadi kubwa ya madini
husuisani Tanzanite soko lake linahamishiwa nje ya nchi badala ya kufanyika hapa
nchini .
Vile vile walisema
kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni waliongia ubia na watanzania kwa kufungua
Kampuni ya kununua madini hapa nchini.
Walisema uwepo wa
Kampuni hizo za kigeni kwenye soko la madini umesababisha ujio wa wawekezaji
wakubwa ndani ya ofisi zao kwa kisingizio cha wataalam na hivyo kuwa chanzo cha
utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kwenda nje ya nchi hususani nchi ya India
na kufanya nchi hiyo iwe kitovu cha uuzaji wa madini ya Tanzanite
duniani.
Kwa upande wa
mwenyekiti wa TAMIDA kanda ya kaskazini,Sammy Mollel alisema kuwa sekta ya
madini hapa nchini imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ,ikiwemo ya wazawa
kutonufaiki na madini badala yake ,wawekezaji ndio wamekuwa wakipewa
kipaumbele,hali inayochangia kwa wananchi kutoona umuhimu wa kuwepo kwa
wawekezaji hapa nchini.
Mollel alisema
kuwa ,wameishauri serikali kupitia wizara
husika,kutazama upya utoaji wa leseni kwa wawekezaji badala yake leseni zitolewe
kupitia kwa kamishna wa madini nchini hatua ambayo itasaidia kuwatambua
wawekezaji moja kwa moja ikiwemo kuwafanyia uchunguzi.
Waliiomba serikali
kufuta leseni za wawekezaji wote wa madini ili watume maombi upya pamoja na
kukamilisha masharti ya serikali ikiwemo kuweka sharti la kakata
madini hapa nchini yanayoanzia gramu 1 na kuaendelea badala ya kuyasafirisha
yakiwa hayajakatwa.
Aidha waliiomba
serikali kuhakikisha kuwa wanawaondoa wawekezaji wa madini toka nje ya nchi
wakipewa mita na serikali yao huku wafanyabiashara wakubwa wa madini wakiwa
hawanufaiki chochote ndani ya nchi yao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia