waziri wa fedha ofisi ya rais Zanzibar Yusuphy Mzee akiwa anabadilisha
mayazo na Makamu wa Rais wa benki ya Maendeleo ya afrika(Afdb) Dr.Kwame
Donkoh katika mkutaano unaoendelea jijini Arusha
Mwenyekiti wa bodi ya chuo kikuu UDMO akiwa anabadilishana mawazo na washiriki wengine katika mkutano wa AfDB
naibu waziri wa fedha tanzania bara Jeneth Mbene kati kati
kushoto kwake Yusuph Mzee waziri wa fedha ofisi ya rais zaizi kulia
wake ni makamu wa rais wa AFDB Dr.Kwame Donkoh
rais wa AfDB Donald Kaberuka akiwa anasalimiana na naibu waziri wa fedha
tanzania bara janeth mbene wakati alipo wasili kutoka nchini kenya
katika mpaka wa namanga
alipokelewa na watu mbalimbali
Watanzania
wametakiwa kujitangaza kiuchumi kupitaia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika(AfDB) ulioanza jijini Arusha ambao umewajumuisha Marais 6, Magavana wa
Nchi mbalimbali za Afrika
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kikuu cha Dodoma Juma Mwapachu
ambapo alisema kuwa hii ni fursa ya pekee kwa Watanzania kushiriki kikamilifu
katika mkutano huu
Mwapachu
alisema kuwa Mkutano huu ni muhimu sana kwa Nchi yetu na unawajumuisha watu
mashuhuri na Si vikao vya Magavana tu pia Umoja wa Mabenki ya biashara ya
Afrika nzima pamoja na vyombo vya habari Mashuhuri
Aliongeza
kuwa katika mkutano huo pia kuna vyombo vya kupima gredi ya Uchumi wa Nchi mbalimbali na mfano
Tanzania Uchumi wake umekuwa ukitolea mfano katika mkutano wa Benki ya
maendeleo ya Afrika
Alisema kuwa
kupitia Benki hii pia wameweza kufadhili ujenzi wa miundombinu ya barabara ya
Namanga hadi Arusha nab ado wapo mbio kuhifadhili barabara ya Moshi hadi Holili
“Kweli
uchumiu wetu unabadilika kiharaka sana,na ukitazama mtikisiko wa kiuchumi
2008-009 ambao kweli kuna nchi ambazo zimetikiswa kiuchumi ”alisema Mwapachu
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania Richard Kasesera alisema kuwa ni
fursa adhimu ya kukuza uchumi kwa Mkoa wa Arusha na kuvitaka vyombo vya habari
kuwa chachu ya kutangaza uchumi wa Tanzania wakati huu Mkutano unapoendelea
Aliongeza
kuwa ni jambo la muhimu kwa vyombo vya habari kuelezea matatizo yetu ya
kiuchumi na kuacha kuzipa kipaumbele habari za vurugu za Zanzibar za vikundi
vichache na kuzipa kipaumbele habari hizo huko ni kuwanyima watanzania kupata
na kuwatia hofu wahisani
Mkutano huu
wenye kauli mbiu Afrika katika Ulimwengu wa utandawazi,changamoto na Fursa
unafanyika kwa siku 4 na kukusanya zaidi ya washiriki elfu mbili
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia