WAJIPANGA KUPANUA SOKO LA VIVYWAJI


Mega trade Investment ltd imejipanga kuongeza wigo wa soko lake la vinywaji vikali katika mikoa yote ya Tanzania na nje ya nchi katika kuwafikia wateja wake.

Hayo yamesemwa na meneja masoko ya kampuni hiyo Mahaligewi Elinae wakati akizungumza na Libeneke la kaskazini kwenye kiwanda hicho maeneo ya Unga Ltd jijini Arusha.

Eilinae alisema kuwa pamoja na kupewa zawadi ya maonyesho ya magari na maandamano kwenye sherehe za may mosi mwaka huu kwa kushika nafasi ya pili wanajipanga kushikilia hnafasi ya kwanza hapo mwakani.

Alisema kuwa kukatika kwa umeme kumekuwa ni tatizo linalowafanya kutoweza kufufikia malengo yao kunakotokana na ongezeko la gharama zisizo za lazima.
Awateja wao kuendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani zina ubora wa hali ya juu na kuwa wao wapo kuwaletea vitu bora kila kukicha.

“sisi tupo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kupanua wigo wa biashara zetu kwani maandalizi yetu yapo kwa wafanyakazi na wateja wetu katika kuongeza sla ndani na la nje”aliongeza Alinae.

Alisema kuwa mwakani malengo yao ni kuongeza wigo na kushinda katika maonyesho ya may mosi na kufanya ushindani japo tumepewa zawadi ambayo siyo yetu kwani sisi hatupo kwenye viwanda vidogo tupo katika makampuni makubwa na hata waandaaji wamekiri kukosea alisema Alinae

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia