BREAKING NEWS

Wednesday, May 23, 2012

 waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr, Emanueli Nchimbi akiwa anamvalisha taji mmoja wa wasaidizi wa kiongozi mkuu  wa dini ya Shri Swaminarayan Mandir Pramamukh Swaming Maharajya kuja kuzindi katika uzinduzi wa msikiti wa dhehebu yao
 waziri wa mambo ya ndani Emanuel Mnchimbi akiwa anaongea katika uzinduzi wa msikiti wa dhebu
 Kiongezi wa dhehebu hili la Shri Swaminarayan Mandir Pramamukh Swaming Maharajyaakiongea na waumini wake
waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr, Emanueli Nchimbi akiwa anamvalisha taji mmoja wa wasaidizi wa kiongozi mkuu  wa dini ya Shri Swaminarayan Mandir Pramamukh Swaming Maharajya kuja kuzindi katika uzinduzi wa msikiti wa dhehebu yao

WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi dk.Emanuel Nchimbi amesema kuwa
serikali imekuwa karibu na Dini ya  Kihindu kupitia dhehebu lao la
Shri Swaminaraya kutokana na dini hiyo kati ya moja ya imani zao ni
mahitaji ya msingi ya binadamu ambayo ni malazi,chakula,afya,maji
yatazamwe kwanza halafu falsafa ya dini ndiyo ifuate.

Waziri huyo aliyasema hayo jana mjini Arusha wakati alipokuwa

akizungumza na waumini wa dhehebu hilo kwa niaba ya Rais jakaya
Kikwete aliyekuwa amealikwa katika uzinduzi wa msikiti huo.

Dk,Nchimbi alisema kuwa endapo mtua au taasisi inapomjali mwenzie

asiye na uwezo,hbari ya sala inakuwa na nguvu zaidi baada ya kuwa
mahitaji hayo yametekelezwa.

"Kwa msingi huo wanaongelea uboreshaji wa  maisha ya binadamu hivyo

serikali inaguswa na kuwataka waendelee kusimamia imani yao maana hii
ni imani yao na siyo yetu ila inawiana na  mtazamo na serikali"alisema

Alisema kuwa wanaiunga mkono na serikali itazidi kuwaunga mkono na

kuwasihi katika shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya kwenye jamii
ikiwemo kuchangia elimu na afya pamoja na mambo mengine wazidishe
zaidi ili ujumbe wao kwa umma ufundishike kwa vitendo.

aliongeza kuwa wamekuwa wakisimamia maadili bora kwa jamii na hakuna

serikali inayotaka kuwa na wananchi wasio na maadili kwani imekuwa ni
changamoto kubwa,ambayo wakiisimamia itasambaa kwa wengine.

Alisema kuwa katika suala zima la kudumisha amani litaweza kufanikiwa

kwa kiwango kikubwa kwani wananchi watakuwa na maadili hasa
ikizingatiwa kuwa dini hiyo imekuwa ikisimamia kikamilifu maadili bora
ya jamii.

Aliwapongeza waumini hao kwa kujenga msikiti ambao una ubora kuliko

ile iliyopo katika mikoa ya Tanga,Dar es Salaam na Mwanza na kuwa
msikiti wa mfano barani Afrika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa msikiti huo hapa nchini Subhasha Patel

alisema kuwa ujenzi wa msikiti huo utaleta manufaa makubwa ikiwa ni
pamoja na kuleta ajira na kwua moja ya kivutio kwa watalii.

Alisema kuwa kwa kila mwaka wanatoa huduma yha afya bure kwa watoto

wasiopingua 17,000 na wengine zaidi ya 3000 kusomeshwa sambamba na
kuwasaidia wazee kupata matibabu.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates