muonekano wa moja ya vyoo vya jengo la mkuu wa wilaya jengo ambalo wafanyakazi wanalalamikia
WAFANYAKAZI
katika jengo la mkuu wa wilaya ya Arusha wamelalamikia ukosefu wa choo kwa muda
mrefu wakidai afya zao zipo hatarini kukumbwa na mlipuko wa magonjwa,kufuatia
choo kilichopo kuziba na kusababisha mazingira ya ofisi hiyo kutapakaa
maji machafu yenye harufu kali na vinyesi .
Suala hilo
limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kupatiwa ufumbuzi huku
wafanyakazi hao wakiendelea kukumbwa na adha ya harufu kali sanjari na
kukanyaga maji machafu kila siku wakati wakiingia ofisini kwao.
Wakizungumza na
waandishi wa habari kwa sharti la kutonukuliwa majina yao na vyombo vya
habari,walisema kuwa adha hiyo imekuwa ikiwakumba zaidi watumishi waliopo chini
ya jengo hilo ,ambapo watumishi walipo juu gorofani wamekuwa wakimwaga
maji na kusababisha choo cha chini kutapisha maji machafu vyenye
vinyesi na kuzagaa eneo la jingo hilo.
‘’kama mnavyoona
hii hali inatisha kwani muda mrefu sana hiki choo kimeziba wenzetu wakimwaga
maji huko juu ,uchafu wote unatoka nje na kutapakaa kila kona vikiwemo
vinyesi ,mipira ya kiume (condom),na pedi za akina mama vinazagaa ovyo’’alisema
mmoja wa watumishi katika jingo hilo idara ya elimu
Wafanyakazi hao
kutoka idara m,balimbali za serikali katika jingo hilo wamedai kuwa wamekuwa
wakipata shida mahala pa kujisaidia na kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta
huduma hiyo ya choo.
Aidha wamedai
taarifa juu ya ubovu wa choo hicho walishaitoka kwa viongozi kadhaa wa wilaya
waliopo katika jengo hilo akiwemo mkuu wa wilaya Raymond Mushi na katibu tawala
wa wilaya Emi Lyimo,bila kupatiwa ufumbuzi .
Kukosekana kwa
huduma ya choo katika jengo hilo kumewakumba watumishi wa idara mbalimbali za
serikali ambao ni pamoja na Baraza la Ardhi wilaya,Ofisi ya mshauri
wa migambo,Hazina ndogo ,Elimu mkoa,Mkaguzi wa elimu kanda ya mashariki,ofisi
ya wazee na ofisi ya mbunge.
Akizungumzia hali
hiyo katibu tawala wa wilaya Emi Lyimo alikiri kupata taarifa juu ya uboivu wa
choo hicho ,lakini alidai kuwa suala hilo lipo juu yak e na tayari taarifa
walishazifikisha kunakohusika ofisi ya katibu tawala mkoa ambaye ndie mwenye
mwenye dhamana ya jengo hilo.
Alisema kuwa hali
ya ubovu wa choo hicho ni ya siku nyingi hata mkuu wa wilaya amekuwa akikumbwa
na adha kutokana na harufu kali inayoingia ofisini kwake na kujikuta akishindwa
kufanyakazi kwa ufanisi,hali ambayo ilimlazimu kuitisha vikao mara kadhaa
kuzungumzia hali hiyo.
Kwa upande wa
katibu tawala mkoa wa Arusha,Everin Itanisa ,baada ya kuhojiwa juu ya ubovu wa
choo katika jengo hilo alidai kuwa taarifa hizo anazo ,kilichokuwa kikikwanisha
kufanyika kwa marekebisho ni ukosefu wa fedha .
Alisema kuwa
mradi wa ukarabati wa choo hicho unagharimu kiasi cha shilingi milioni 12 na
ofisi yake haikuwa na fedha ila wamepata nusu yake baada ya kuamua kuachangisha
katika idara zote katika ofisi ya mkuu wa mkoa, kutokana na serikali kutokuwa
na fedha.