wapili kushoto afisa uhusiano wa msikiti wa Shri Swaminarayan ndugu Kaushik Vasan akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa msikiti huo
apa afisa uhusiano wa Shri Swaminarayan Mandir akifafanua jambo kuhusiana na mkubwa wao mbele ya waandishi wa habari
waandishi wakiuliza maswali
wamama wa wenyeasili ya kiasia wakiendelea na maandalizi ya urembo mbalimbali za maua
wakiendelea kuandaa maua kwa ajili ya kurembea
Afisa husiano akionyesha baadhi ya urembo uliotolewa india kwa ajili ya msikiti huo
Waandishi wa habari ak iwemo Jamila Omary wa chanel Ten,Pamela Mollel wa majira wakiwa wanaangalia magari kwa maaalumu yaliyotengenezwa ajili ya kubeba vivutio mbalimbali vya dini hiyo
Muonekano wa msikiti kwa nje
Dini ya hindu kupitia dhebhebu la shri swaminaraya
imeahidi kutoa elimu kwa waumini wake pamoja wananchi wasiowahumini
kuhusiana na sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika mapema
mwezi agosti.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisa uhusiano wa dhehebu hilo Kaushik Vasan
alisema kuwa dini yao ipo tayari kutoa ushauri kwa waumini wao pamoja na
wananchi kwa ujumla ili kuweza kubaini nini maana ya sensa ambapo pia
watawahamasisha wananchi hao kushiriki zoezi hili siku hiyo.
Alisema
kuwa pia kwa kutumia sherehe hizi za uzinduzi wa jengo lao la msikiti
wao ambao wameujenga jijini hapa ambao wanatarajia kuzindua jana (leo)
watahamasisha watu wote ambao watahudhuria sherehizo kushiriki zoezi
hili.
Vasan
alisea kuwa kutokana na umuhimu wa sensa hiyo ya watu na makazi
wataisaida serikali katika kuhamasisha waumini wake na wakazi wa jiji
hili kwa ujumla juu ya umuhimu wa kujiandiksha kwakati wa sensa.
Aongelea
uzinduzi wa msikiti huo alisema kuwa mgeni rasmia anatarajiwa kuwa
Ghanshyam Charan Swami ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa kiongozi wao mkuu
wa dini hiyo ambaye ni HDH,Pramukh Swami Maharaj(91) aishiye nchini
India.
Alibainisha
kuwa katika uzinduzi huo wanatarajia zaidi ya wageni 800 kutoka nje ya
nchi ambao watafika kusherekeapamoja zoezi hilo ,huku akibainisha kuwa
mbali na masuala ya kiima wanajikita pia katika kusaidia jamii ikiwepo
kupanda miti kwa ajili ya mazingira ,kutoa huduma mbalimbali za kijamii
kama vile kusaidia hospitali mbalimbali vifaa ,pamoja na kuwasomesha
watoto yatima na wale ambao wanaishi katika mazingira
hatarishi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia