BREAKING NEWS

Wednesday, May 23, 2012

WAJASIRIA MALI 300 KUSHIRIKI MAONYESHO YA BIDHAA TANGA

Zaidi ya wajasiriamali 300 kushiriki maandamano na maonyesho ya bidhaa za ndani  yatakayofanyika may 30-juni4 mwaka huu katika viwanja vya Tangamano  jijini Tanga.

Akizungumza na libeneke meneja wa shirika la viwanda vidogo vidogo(SIDO)mkoani hapa Isidori Kiyenze alisema kuwa maonyesho hayo yanalenga kujenga msingi wa viwanda vyetu vya kati na vidogo katika kutafuta masoko ya nje ya nchi na ndani.

Kiyenze alisema kuwa kumekuwapo kutokujiamini kwa wajasiriamali wa ndani kupeleka bidhaa zao katika maonyesho mbali mbali ya nje hivyo wanaona ni wakati wa kuwasogeza na kujijenga katika wakati huu wa soko huria.

Akaongea kuwa maonyesho hayo yataambatana na maandamano yatakayoanzia katika uwanja wa Mkwakwani na kuishia katika viwanya vya tangamano Kauli mbiu ya maonyesho hayo mwaka huu ni “Sido kwa Teknolojia  na Masoko Mapya”aliongeza Kinyenze.

Mikoa itakayoshiriki ni pamoja na wenyeji Tanga,Kilimanjaro ,Arusha na Manyara na kuwataka wajasiriamali  mbali mbali kutoka sehemu za nchi hii  kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo sanjari na wanachi wa mikoa hiyo.

“Tupo kaitka mchakato wa mwisho wa kuandaa maonyesho ya wajasiriamali wa jumuiya ya Afrika ya mashariki(EAC) kwa kuzishirikisha nchi 5 za jumuiya hiyo yatakayofanyika mwakani”alisema Isidori.

Akawataka wajasiriamali nchini kutumia maonyesho haoy kujipima viwango kabla ya kushiriki maonyesho ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates