Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumanne, imethitisha
adhabu za warufani wawili na kumpunguzia mwingine mmoja, Meja Aloys
Ntabakuze adhabu ya kifungo cha maisha jela hadi miaka 35.Wakati huohuo
kesi ya msomi,Leon Mugesera aliyerejeshwa nchini Rwanda, Januari mwaka
huu kutoka Canada itafikishwa mahakamani tena Mei 24.
ICTR
Ataka Gatete atiwe hatiani kwa kosa la kula njama: Jumatatu Mei 7,
Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda (ICTR) ilisikiliza rufani ya Jean Baptiste Gatete ambapo
mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo imtie hatiani pia kwa shitaka
la kula njama za kufanya mauaji.Machi 29, 2011 Gatete alitiwa hatiani
kwa kuhusika na ya Watutsi katika maeneo matatu tofauti Mashariki mwa
Rwanda kati ya Aprili 7 na 12, 1994. Alihukumiwa kifungo cha maisha
jela. Kwa upande wake, mawakili wa utetezi waliomba mteja wao apunguziwe
adhabu.
Ntabakuze apunguziwa kifungo cha maisha hadi miaka 35 jela: Aliyekuwa
na bahati ya pekee katika rufaa tatu zilizotolewa hukumu Jumanne na
Mahakama ya Rufaa ya ICTR ni Meja Aloys Ntabakuze ambaye amepunguziwa
adhabu kutoka kifungo cha maisha jela hadi miaka 35. Ntabakuze alitiwa
hatiani kwa mauaji ya kimbari,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa
kivita Desemba 18, 2008 kwa sababu ya askari waliokuwa chini ya mamlaka
yake kushiriki kwenye mauaji katika maeneo matatu katika jiji
laKigalimwaka 1994.
Siku hiyo pia Mahakama ilithibitisha adhabu walizopewa warufaani
wawili na mahakama ya ICTR. Wahusika ni pamoja na Afisa wa zamani wa
jeshi la Rwanda Luteni Idelphonse Hategekimana ambaye ataendelea
kutumikia adhabu yake ya kifungo cha maisha jela.
Hategekimana
alipatikana na hatia kwa makosa ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi
ya binadamu.Mwingine aliyethibitishiwa adhabu yake ni mfanyabiashara
Gaspard Kanyarukiga aliyetiwa hatiani Novemba 1, 2010 kwa makosa ya
mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi kwa kushirikiana na wengine,
kubomoa kanisa la Nyange, Magharibi ya Rwanda, Aprili 16, 1994.Watutsi
wapatao 2000 waliokuwa wanapata hifadhi katika kanisa hilo waliuawa.
RWANDA
Mugesera mahakamani Mei 24: Msomi aliyerejeshaRwandaJanuary mwaka
huu, Leon Mugesera atarejea mahakamani Mei 24.Mgesera anashikiwa kwa
makosa ya kuchochea mauaji ya kimbari katika hotuba aliyoitoa katika
kkutano wa chama chake cha siasa mwaka 1992. Aprili 17,Mahakama Kuu
nchiniRwandailituplia mbali maombi yake ya kutaka kesi yake isikilizwe
kwa lugha ya Kifaransa na badala yake mahakama iliamuru isikilizwe kwa
lugha ya Kinyarwanda.
WIKI HII
ICC
Wiki hii, Jumanne, Mei 15, Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
(ICC) itasikiliza hoja za mwisho katika kesi inayowakabili waasi wawili
wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), German Katanga na
Mathieu Ngudjolo. Watu hao wanashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu
na uhalifu wa kivita kwa kuhsika kwao katika mashambulizi ya eneo la
Bogoro, Ituri, Mashariki mwa DRC, Februari 24, 2003 ambapo watu zaidi ya
200 waliuawa.
SCSL
Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL) wiki hii, Jumatano Mei 16,
itasikiliza hoja za mapendekezo ya adhabu anayostahili kupewa, Rais wa
zamani wa Liberia, Charles Taylor (64) aliyetiwa hatiani na mahakama
hiyo kwa makosa 11 ya vita na uhalifu dhidi ya binadamu.Alikuwa
anahusika kwa kuwasaidia waasi wa Seirra Leone katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2000. Mwendesha mashitaka kapendekeza
ahukumiwe kifungo cha miaka 80 jela.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia