Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumanne imehitimisha kupokea ushahidi maalum katika kesi inayomhusu mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari anayesakwa vikali na mahakama hiyo, Felicien Kabuga, kesi kama hiyo pia dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, Augustin Bizimana aliahirishwa hadi Juni 25, 2012.
‘’Upokeaji wa ushahidi maalum katika kesi ya Kabuga ulimalizika na jumla ya mashahidi sita walijitokeza kumtetea mtuhumiwa,’’ Msemaji wa ICTR, Roland Amoussouga aliliambia Shirika la Habari la Hirondelle Jumatano.
Wakili wa zamu anayemwakilisha Kabuga katika kesi hiyo, Bahame Nyanduga alianza kuwasilisha mashahidi wa utetezi wa mteja wake Aprili 23, 2012. Mwendesha mashitaka kwa upande wake alianza kuita mashahidi Mei 23,2011 na kuhitimisha Oktoba 28, 2011.
Kabuga anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari, kula njama za kufanya mauaji hayo, au kushiriki mauaji hayo, kujaribu kufanya mauaji ya kimbari, uchochezi na ukatili dhidi ya binadamu hususan ni utesaji na kuteketeza kizazi.
Amossouga pia alisema kwamba ICTR imeahirisha usikilizaji wa ushahidi maalum wa upande wa utetezi katika kesi ya Bizimana hadi Juni 25. ‘’Kuhusu Bizimana, usikilizaji wa ushahidi umeahirishwa hadi Juni 25, 2012 kwa kuwa shahidi wa tatu wa utetezi alisema hataweza kupatikana kabla ya Juni 20,’’ Msemaji alifafanua.
Usikilizaji maalum wa ushahidi wa kesi hufanyika kwa lengo la kukusanya na kuhifadhi baadaye iwapo watuhumiwa husika watatiwa hatianiushahidi husika ili kuweza kutumika .

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia