Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari
JESHI la polisi mkoani Arusha limetangaza kumsaka popote
alipo hadi uvunguni mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua
Nassar(26)alimaarufu dogo janja likimtuhumu yeye na wenzake kutenda kosa la
kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa chadema uliofanyika jumamosi
iliyopita katika viwanja vya NMC jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Naibu kamishina wa polisi nchini,Isaya Mngulu
alimtaka mbunge huyo kujisalimisha polisi hadi leo saa 12 jioni na baada ya
hapo litaanzisha msako mkali wa kumkamata popote alipojificha,baada ya jitihada
za kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi
kuwa kushindikana baada ya kuwa imezimwa.
Mnguli alisema kuwa pamoja na kumsaka mbunge huyo,polisi
inawahoji makada kadhaa wa chadema ,akiwemo Ally Bananga aliyehamia chadema
akitokea ccm,mwenyekiti wa Bavicha Taifa,John Heche na Alphonce Mawazo ambaye pia amejiunga na
chadema akitokea ccm.
Alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitamka maneno
ya uchochezi yanayohatarisha uvunjifu wa amani na kuyataja baadhi ya maneno hayo kuwa
ni kutaka mikoa kadhaa ijitenge kama sudani kusini.
Aliyataja maneno hayo kuwa ni’’iwapo polisi haitawakamata watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa
chadema kata ya Usa River,Msafiri Mbwambo,mkoa wa Arusha na baadhi ya mikoa kanda
ya ziwa itajitenga kama Sudani kusini na
kwamba Rais Kikwete hata kanyaga Arusha.
Maneno mengine ni Ridhiwan Kikwete anawapenzi wengi wa
kike ambao amekuwa akiwatambulisha kwa baba yake(kikwete) na Kikwete amekuwa
akiwateua na kuwapa nyadhifa muhimu serikalini na kuifanya serikali ya
Kiswahiba.