Mbele ya Mahakama Maalum ya
Sierra Leone (SCSL) wiki hii Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor
aliilaimu Marekani kwa kula njama dhidi yake wakati katika Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) majaji walisikiliza hoja za mwisho za
mwendesha mashitaka katika kesi inayowakabili GermanKatanga na Mathieu
Ngudjolo.
SCSL
Taylorailaumu Marekani kwa kula njama dhidi yake: Rais wa zamani
waLiberia, Charles Taylor Jumatano wiki hii aliilaimu Marekani kwa kula
njama za kumwodoa madarakani na kumshitaki alipopewa nafasi na Mahakama
Maalum ya Sierra Leone (SCSL) kusema neno la mwisho katika kesi yake
kabla ya siku ya hukumu. Mwendesha mashitaka kapendekeza ahukumiwe
kifungo cha miaka 80 jela kwa kuzingatia uzito wa makosa na ukatili
uliofanyika nchini Sierre Leone wakati wa uhalifu huo. Lakini mawakili
wake waliileza mahakama kwamba adhabu hiyo ni sawa na kumpatia kifungo
cha maisha jela.
ICC
Mwendesha mashitaka atoa hoja za mwisho kesi yaKatanga:Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imesikiliza hoja za mwisho za upande
wa mwendesha mashitaka katika katika kesi inayowakabili waasi wawili wa
zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), German Katanga na
Mathieu Ngudjolo. Akiwasilisha hoja zake, mwendesha mashitaka alidai
kwamba katika eneo la Bogoro, waasi waliua kila mtu.Watu hao
wanashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita kwa
kuhusika kwao katika mashambulizi ya eneo la Bogoro, Ituri, Mashariki
mwa DRC, Februari 24, 2003.
Ocampo ataka kamanda wa FDLR akamatwe: Jumatatu wiki hii,Mwendesha
mashitaka wa ICC Luis Mreno Ocampo alitoa hati ya kukamatwa kwa kamanda
kundi la waasi la FDLR, Sylvestre Mudacumura.Anatuhumiwa kwa mashitaka
matano ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanyika
katika majimbo ya Kaskazini na Kusini mwa Kivu, DRC.
ICTR
Ushaidi maalum kesi ya Bizimana wapokelewa: Mahakama ya Kimataifa ya
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu wiki hii ilianza kupokea
ushahidi maalum wa utetezi katika kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa
Ulinzi waRwanda, Augustin Bizimana ambaye bado anasakwa.
WIKI IJAYO
ICTR
Majaji na pande zinazohusika katika kesi ya mauaji ya kimbari
yaRwandainayowakabili Waziri wa zamani wa Ulinzi waRwanda, Augustin
Ngirabatware Jumatatu ijayo wataanza ziara nchiniRwandaya kutembelea
maeneo yanayosadikiwa kutendeka kwa uhalifu mwaka 1994.
RWANDA
Mugesera mahakamani Mei 24: Msomi aliyerejeshwaRwandaJanuary mwaka
huu, Leon Mugesera atarejea mahakamani Mei 24, Alhamisi ijayo.Mgesera
anashikiwa kwa makosa ya kuchochea mauaji ya kimbari katika hotuba
aliyoitoa katika mkutano wa chama chake cha siasa mwaka 1992.
ICC
Mawakili wa utetezi katika kesi
inayowakabili waasi wawili wa DRC, German Katanga na Mathieu Ngudjolo
watawasilisha hoja zao za mwisho mbele ya ICC.
Habari zote na mdau wa libeneke la kaskazini Nicodemus Ikonko.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia