CHADEMA KUZINDUA VUA GAMBA VAA GWANDA KESHO NMC

nembo ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kesho kinazindua operesheni maalum vua gamba vaa gwanda kwenye vianja vya NMC kiuanzia saa nane mchana ambapo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe anatazamiwa kuwa mgeni Rasmi
Pia kwenye mkutano huo aliyekuwa mwenyekit wa jumuiya yua vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM), James Millya pamoja na wana chama wengine waliojitangaza kujivua magamba wanatazamiwa kupewa kadi za uwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Mbali na mwenyekiti wa chama hicho kuhudhuria katika mkutano huo pia kutakuwa na viongozi mbalimbali wa chama wa mkoa na taifa ambao watakuwepo  wakiongozwa pia na mbunge wa jimbo la Arusha mjini aliyeenguliwa Godbless Lema

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post