kikundi cha ngoma za kimasai wakiingia kusherehesha
Wamasai wakiwa stagini wakiimba nyimbo zao za asili ya kimasai kwenye tamasha hilo lililokuwa limeandaliwa na Endeleza Foundatio. |
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi akipiga ngoma kama ishara ya kufungua tamasha hilo la kitamaduni vs Bongp Fleva kwenye viwanja vya Mandela Pasua Mjini Moshi. |
Hapa Inspekta na mwenzake wakifanya mambo kuwapagawisha wananchi na vikundi mbalimbali vya sanaa vilivyofika kwa siku ya leo
Hapa
Mkuu huyo wa Wilaya Dr Ibrahimu Msengi akiwa na vikundi vya ngoma
mbalimbali za kitamaduni kabla ya kufungua rasmi tamasha hilo
Akizindua tamasha hilo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr Ibrahim Msengi amesema Moja ya mambo ambayo yanaendelea kuubomoa kama siyo
kutokomeza kabisa utamaduni wa
watanzania ni pamoja na utandawazi ambao umekuwa ukichangia wananchi hususani
vijana kushabikia tamaduni za magharibi kusahau tamaduni za kiafrika.
Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza na
umati wa wananchi waliohudhuria tamasha hiloambalo limehusisha nyimbo
mbalimbali ikiwemo zile za kiasili
ambazo zinazounzi utamaduni wa kitanzania na kufanyika kwenye viwanja
vya mandela kata
ya pasua manispaa ya moshi amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa
waannchi kuendelea kuuenzi utamaduni wao
Amesema kuwa mahali popote
utakapoenda utamaduni hutumika kama kitambulisho kama itakuwa ni lugha
fulani au mavazi au chochote kile ambacho kitakuwa kinatambulisha
utamaduni wako basi inakuwa ni kitambulisho kwako.
.
Kwa upande wakeMratibu wa tamasha hilo Ismail
Mnikite kutoka endeleza foundation tamasha ambalo limehudhuriwa na ngoma za makabila
mbalimbali amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha, kuendeleza na
kuimarisha zaidi utamaduni wetu baada ya kuadhiriwa kwa kiasi kikubwa na
utandawazi.
habari na picha kwa hisani ya Tanzania leo sauti ya watanzania
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia