WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUWAKARIMU WAGENI


Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya
Wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na wa mikoa jirani wametakiwa kuwakarimu na kuwapokea vyema wageni wanatarajiwa kuja kushiriki katika mkutano wa benki ya dunia pamoja na mkutano wa Karibu fair unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini hapa.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa jumba la kimataifa la mikutano (AICC) Elisilia Kaaya wakati alipokuwa akingea na Libeneke la kaskazini  leo ofisini kwake.

Alibainisha kuwa  kwakuwa jiji la Arusha linatambulika ni sehemu ya mikutano hivyo wananchi wa mkoa huu waendelee kuwapokea wageni kwa ukarimu wao kwani iwapo watawapokea wageni hawa kwa bashasha basi itakuwa ndio njia moja wapo ya kuwahaasisha wageni hawa kuleta mikutano mingi mkoani hapa.

“napenda kuwaambia wananchi wa mkoa wa arusha pamoja na ile mikoa ya jirani wawapokee wageni hawa ambao wanatoka nchi za nje na wengine hapa hapa nchini kwa ukarimu wao wote kama wanaarusha wawaonyeshe bashasha zote ili wakienda waweze kufikiria ukarimu wetu na walete mikutano mingine kwani kwa kadri wanavyoleta mikutano ndio ivyo wanazidi kutuongezea pato letu la taifa na pia ata sisi wenyewe tunafanya biashara ivyo tunaongea pato letu binafsi”alisema Kaaya.

Alisema kuwa mpaka sasa maandalizi yanaendelea vyema  na ukarabati wa ofisi ambazo zitatumika unaendelea na wanatarajia hadi ifikapo May 15 nusu au robo tatu ya ukarabati itakuwa imekamilika na mbali na ukarabati wa majengo na ofisi za AICC pia katika maeneo ya shughuli za kiofisi nazo zitakuwa zimekamilika.

Aliliambia libeneke kuwa wanatarajia watu 2000 kuuthuria katika mkutano huo na watatumia vyumba vyote vya AICC na pia havitatosha kwa kuwa ni wengi ivyo wengine wanatarajia kutumia hoteli nyingine kwa ajili ya mikutano na mambo mengine.
“pia napenda kuwajuza wananchi kwakweli maandalizi ni mazuri kwani hata katibu mkuu wa Afrika Development Bank alivyokuja kukagua alisifia maandalizi haya kwa ufupi ameridhishwa nayo,kwani kwa muonekano alionekana kuondoka na faraja kubwa”alibainisha kaaya
Aidha aliwapongeza TATO kwakusogeza mkutano mmoja wa Karibu fair mbele kwani alibainisha kuwa wameonyesha uzalendo wa hali ya juu na pia wametoa fursa ya nchi kuweza kuhudumia vizuri mkutano mmoja mmoja.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post