BREAKING NEWS

Thursday, May 24, 2012

WASICHANA WA JAMII YA KIFUGAJI WATAKIWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

 wanafunzi wa jamii ya kimasai waisikiliza mada kwa makini
Wasichana wa jamii ya kifugaji wilayni Monduli mkoani Arusha,wametakiwa kupenda kusoma masomo ya sayansi iliyaweze kunufaika na teknolojia ya mbali mbali na kuisaidia jamii yao.

Meneja wa kanda ya kaskazini wa mamlaka ya mawasiliano(TCRA)Annete Matindi alitoa wito huo katika seminwa ya maadhimisho ya wiki ya mawasiliano simu na habari jamii katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok wilayani Monduli.

Alisema wakati mamlaka hiyo ikiwa imejipanga kufikisha huduma za teknolojia ya mawasiliano hadi vijijini wasichana wa jamii ya wafugaji wanafursa kubwa ya kunufaika na huduma hizo.

“Huduma za mawasiliano sasa zinafika vijijini hivyo,kuna fursa kwenu kuzitumia katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili”alisema Matindi

Matindi alisema TCRA imejipanga kuhakikisha huduma ya mawasiliano ya Intaneti inawafikia wananchi wengi ambao wanaishi vijijini ili waweze kuitumia kujifunza mambo mbali mbali kikiwemo kilomo cha kisasa na utaalamu wake.

Awali mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga alitowa wito kwa wasichana wa jamii hiyo ya kifugaji kujikita kusoma masomo ya sayansi katika kuipelekea jamii teknolojia mbali mbali watakazo kuwa wamejifunza

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates