Meneja wa kampuni ya bia kanda ya kaskazini Wilderson kitio akiwa anamkabidhi hundi ya shilingi milioni tatu mwenyekiti wa APC Abraham Gwandu kulia
Kampuni ya bia ya TBL imekabidhi
msaada wa shilingi milioni tatu kwa chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha
(APC) kwa ajili ya kusherekea siku ya uhuru.
Akikabidhi msaada wa fedha hizo meneja masoko wa TBL kanda ya kaskazini
Wilderson Kitio alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa msaada huo wa fedha ili
kuwezesha siku hiyo ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari kufana kwa mkoa
wa huu.
Alibainisha kuwa kama tbl wamekuwa wakishirikiana sana na waandishi
wahabari katika kazi mbalimbali hivyo hata katika siku hii yao ya kusherekea
lazima washirikiane.
"na sisi kama kampni ya bia ya TBL taendelea kushirikiana na wanahabari na
mchango huu autaishia hapa balitutakuwa tunachangia kila mwaka"alisema
Kitio.
Akipokea msaada huo mwenyekiti wa APC Abrahamu Gwandu aliwashukuru kampuni
hii na kubainisha kuwa wamewasaidia sana katika kufanikisha siku hii na kusema
kuwa wataendelea kuwa na ushirikiano nao katika mambo mbalimbali.
Alisema kuwa siku hii itafanyika may 3 katika ukumbi wa goldenrose na
utashirikisha wandishi wahabari pamoja na wadahu wa habari ambapo kutakuwa na
mada mbalimbali ambapo alisema kuwa katika sikul hii kutakuwa na vitu mbalimbali
ikiwemo mafunzo kwa waandishi wa habari.
Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na kujikumbushia sheria za uhandishi
wahabari ,jinsi ya kujikwamua katika uchumi,maswala ya sheria za uhandishi na
nyingine nyingi
Alibainisha kuwa mpaka sasa wathamini waliojitokeza kuthamini siku hii ni
wawili pamoja na muungano wa vyombo vya habari tanzania huku akibainisha kuwa
nafasi kwa wathamini wengine ipo wazi.
|