Monday, May 21, 2012
BAVICHA ARUSHA WATOA TAMKO KUHUSIANA NA SHIBUDA
Posted by woinde on Monday, May 21, 2012 in | Comments : 0
Baraza la Vijana CHADEMA mkoa wa Arusha(BAVICHA) bavic Taarifa kwa umma BAVICHA mkoa wa Arusha,inaunga mkono Tamko la BAVICHA Taifa,juu ya hatua ya Mh Shibuda kutoa Tamko la kukidhalilisha chama mbele ya viongozi wa ccm.Kimsingi BAVICHA hatuna tatizo na nia ya Mh Shibuda kugombea Urais,bali kauli yake kuwa chama pekee kinachoweza kushika dola ni ccm.
BAVICHA tunalaani kauli hii,na tunapenda kuujulisha umma wa Tanzania kuwa CHADEMA imejipanga kuchukua Dola,ina mfumo mzuri wa kiuongozi kutoka chini,hadi Taifa,ni chama pekee chenye Katiba bora na kinachotetea kwa vitendo masilahi ya umma,ni tumaini pekee kwa mamilioni ya Watanzania Kimsingi Mh Shibuda anaweza kuwa anatumiwa na ccm kuvuruga FOCUS yetu,kutokana na operesheni Vua Gamba Vaa Gwanda ambayo imekuwa na mafanikio makubwa sana,ambapo maelfu ya viongozi wa ccm wanahamia CHADEMA,huu ni mkakati wa ccm kumtumia Shibuda,tunawaambia kuwa kamwe hatutapoteza Focus yetu,na tumeshtukia mpango huu mapema,tunasonga mbele hadi kieleweke.Chama chetu kimepita katika mapambano na changamoto mbalimbali.
Ni chama pekee ambacho kimewahi kuchukua maamuzi magumu na kubaki imara,katika hili la Mh Shibuda tunaomba chama kichukue maamuzi magumu,hata kwa gharama ya jimbo.
Ukiwa na askari katika kikosi chako ambaye anaamini majeshi ya adui ni bora zaidi na yanastahili kushinda vita askari huyo anakuwa ni msaliti na anapofanya kazi au jitihada ya kutaka adui ashinde kijeshi huo ni uhaini.
Shibuda kutangaza kuwa anataka kugombea Urais kupitia CHADEMA mwaka 2015 siyo tatizo.
Tatizo ni kukidhalilisha chama mbele ya ccm, Imetolewa na Nanyaro EJ Mwenyekiti BAVICHA MKOA WA ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia